Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA

Niger yaendeea kukumbwa na jinamizi la mauaji

Washukiwa wa kijihadi wamewauwa wanakijiji 10 waliokuwa wamekwenda kuswali sala ya jioni katika jimbo la Tillaberi, Magharibi mwa Niger.

Washambuliaji waliwasili kwenye kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kuwafyatulia risasi, watu waliokuwa msikitini.
Washambuliaji waliwasili kwenye kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kuwafyatulia risasi, watu waliokuwa msikitini. AFP Photo/BOUREIMA HAMA
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wanasema, shambulizi hilo lilitokea siku ya Jumatatu katika kijiji cha Abankor karibu na mpaka wa Niger, Mali na Burkina Faso.

Washambuliaji hao waliwasili kwenye kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kuwafyatulia risasi, watu waliokuwa msikitini.

Baada ya tukio hilo, viongozi wa jimbo la Tilaberi wamepiga marufuku usafiri wa pikipiki katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo katika jitihada za kupambana na mashambulizi ya mara kwa mara yanayowalenga raia na wanajeshi.

Tangu mapema mwaka 2021, wanajihadi wameendelea kutekeleza mashambulizi katika eneo la Tiberi ambalo linakaliwa na jamii za watu kutoka makabila ya Djerma, Fulani, Tuareg na Hausa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.