Pata taarifa kuu
NIGER

Niger: Mikoa sita yaathiriwa na ugonjwa wa kipindupindu

Uncerf, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kukabiliana na magonjwa ya kuambukia, limetoa zaidi ya euro milioni 7 kusaidia Niger kukabiliana na mafuriko na ugonjwa wa kipindupindu.

Wagonjwa wakitibiwa baada ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Wagonjwa wakitibiwa baada ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Siku silizopita, Umoja wa Ulaya ulitoa karibu euro 300,000 kupambana na ugonjwa huu. Kesi ya kwanza ya kipindupindu ilitangazwa mwishoni mwa mwezi Machi na licha ya majibu yaliyowekwa haraka na mamlaka, kati ya mikoa nane ya nchi hiyo, sita inaathiriwa na janga hilo.

Kipindupindu huambukizwa kupitia maji yasiyo safi. Mafuriko yaliyosababishwa na msimu wa mvua yalisababisha kuongezeka kwa janga hilo. Katika kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo, mamlaka na mashirika yasiyo ya kiserikali yanalenga, pamoja na mambo mengine, kuzidisha uhamasishaji kuhusiana na hatua za kujikinga, kwa kuelimisha jamii.

“Kuna habari kutoka kwa viongozi na maimamu, mapadre na waganga wa kienyeji. Tulilenga pia wachukuzi, kwa sababu wakati mtu anaumwa, wanakuwa wamefahamu dalili za ugonjwa huo, na kuweza kutoa msaada wao wa kumsafirisha mginjwa hadi hospitali. Katika kiwango cha maeneo ya visiwa, ni waendeshaji mashua, ndio wanaofahamishwa ili waweze kufanya mipangilio wakati wa usafirishaji wa wagonjwa walioathirika ”, amebaini Dk Mossi Alhassane Maiga, mratibu wa afya wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Niger.

Lakini, katika eneo la zaidi ya kilomita za mraba milioni 1.2, changamoto ni kubwa na uwezo bado hautoshi, kwa upande wa Dkt Issa Malam Kanta, mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la matibabu, ALIMA, nchini Niger amesema: "Kuna pia watu kucheleweshwa kupelekwa katika vituo ambavyo tumetenga. Katika jedwali la kipindupindu, kuna kutapika hasa na kwa kuwa ni katika msimu wa mvua, inaweza kumfanya mtu apatwe na magonjwa mengine, kama malaria. Pia kuna shida kwa baadhi ya maeneo kwa sababu ya ukosefu wa usalama na inakuwa ni vigumu kwenda unakotaka. "

Leo, wahudumu wa mashirika ya kutoa msaada yanabaini kwamba zaidi ya visa 4,800 vya ugonjwa wa kipindupindu vimeripotiwa, ikiwa ni pamoja na vifo 151.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.