Pata taarifa kuu
NIGER

Kipindupindu chaua watu zaidi ya 100 Niger

Watu 104 wamefariki dunia nchini Niger kufuatia mlipuko wa ugonjwa kipindupindu kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita kwa mujibu wa Wizara ya afya nchini humo.

Mvua kubwa inayosababisha mafuriko inayoendelea kunyesha tangu mwezi Juni, inaelezwa kuwa sababu kubwa ya janga hili.
Mvua kubwa inayosababisha mafuriko inayoendelea kunyesha tangu mwezi Juni, inaelezwa kuwa sababu kubwa ya janga hili. © Tchadinfos.com
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya inasema watu wengine 2,874 wanasumbuliwa na kipindupindu, huku jiji kuu Niamey, likiathiriwa zaidia.

Tarehe 19 Agosti, visa 845 na vifo 35 viliripotiwa katika mitaa kadhaa jijini Niamey, huku majimbo sita pia yakiathiriwa, ikiwemo mipaka ya nchi hiyo na Nigeria.

Jimbo la Tillabér, linalopakana na Burkina Faso na Mali, eneo ambalo limekuwa likishuhudia mashambulizi ya kijihadi, pia limeathiriwa.

Mpaka tarehe moja mwezi Septemba, vifo vingine 104 viliripotiwa na wagonjwa zaidi ya Elfu Mbili na Mia nane.

Watu walioathiriwa zaidi ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 37 wakati huu, Shirika la Madaktari Wasiokuwa na mipala, MSF, Umoja wa Ulaya na Ule wa Mataifa ukiendelea kutoa elimu kwa watu nchini humo na kusambaza maji safi ya kunywa.

Mvua kubwa inayosababisha mafuriko  inayoendelea kunyesha tangu mwezi Juni, inaelezwa kuwa sababu kubwa ya janga hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.