Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA

Mashambulizi dhidi ya raia yaongezeka Magharibi mwa Niger

Nchini Niger, mauaji mapya ya raia yametekelezwa magharibi mwa nchi na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi. Watu wasiopungua 37 waliuawa Jumatatu alasiri katika shambulio huko Darey-Daye, kijiji kilicho kilomita 40 mashariki mwa mji wa Banibangou, karibu na mpaka na Mali.

Kijiji cha Songhai katika mkoa wa Tillabéri nchini Niger.
Kijiji cha Songhai katika mkoa wa Tillabéri nchini Niger. De Agostini via Getty Images - DEA / N. CIRANI
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yalitokea katika eneo la mkoa wa Tillabéri ambapo ukatili unaofanywa na makundi ya wanamgambo wa Kiislam wenye silaha umeongezeka tangu mwanzoni mwa mwaka.

Kulingana na shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch, zaidi ya raia 420 wameuawa magharibi mwa nchi tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa. Kijiji hiki kinachopatikana kilomita 40 kutoka mji wa Banibangou ni kwa mara ya pili kinashambuliwa katika kipindi cha miezi 6 na watu wenye silaha wakiwa kwenye pikipiki.

Mwanzoni mwa mwaka, familia 250 zilikuwa zinaishi katika kijiji hiki, lakini watu wasiozidi mia moja ndio wanaishi huko, amebaini mmoja wa maafisa katika kijiji cha Darey-Daye.

Mashambulio mashambani

Afisa huyu anakiri kuwa hata yeye pia amekimbia eneo hili kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu raia wamekuwa wakilengwa zaidi, amesema Adamou Oumarou, mwanaharakati wa shirika moja la kiraia kutoka Tillabéri.

“Leo, wanatumia fursa ya kufanya shughuli mashambani kwa kwenda kuua raia. Hapo awali, ukatili huo ulikuwa ukitekelezwa katika vijiji. Sasa leo unafanyika mashambani na hatujui ni kwa sababu gani. Mwanzoni askari ndio walikuwa wanalengwa na mashambulizi hayo katika mkoa huo. "

Makundi yenye silaha ya wanamgambo wa Kiislam yanaonekana kupigana vita dhidi ya raia, limebaini shirika la Human Rights Watch. Wanawake, wakuu wa vijiji, maimamu, na watoto wengi ni miongoni mwa wahanga wa mauaji hayo.

Lazima jeshi letu lipewe vifaa vya hali ya juu ili tuweze kuondokana na zimwi hili la mauaji dhidi ya raia, amesema Amadou Oumara, akihojiwa na Alexandra Brangeon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.