Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Macron kukutana na mamia ya vijana kutoka Afrika

Ufaransa siku ya Ijumaa, inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa nchi hiyo na mataifa ya bara la Afrika, unaolenga kuimarisha mahusiano kati ya Paris na Afrika.

Rais Macron amewaalika mamia ya vijana wanaojihusisha na biashara, michezo na wasanii kutoka Afrika kukutana siku ya Ijumaa wiki hii.
Rais Macron amewaalika mamia ya vijana wanaojihusisha na biashara, michezo na wasanii kutoka Afrika kukutana siku ya Ijumaa wiki hii. Ludovic MARIN POOL/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron anatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu ambao utafanyika katika mji wa Kusini Montpellier, lakini hautahudriwa na viongozi wa mataifa ya Afrika.

Badala yake, rais Macron amewaalika mamia ya vijana wanaojihusisha na biashara, michezo na wasanii.

Afisa kutoka Ikulu ya rais jijini Paris ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kuwa rais Macron atatumia mkutano huo kuwasikiliza vijana kutoka barani Afrika na kufahamu fursa na changamoto zinazowakabili katika masuala ya kiuchumi, tamaduni na siasa.

Tangu mwaka1973, Ufaransa ilikuwa ikifanya mikutano kama hii na viongozi wa Afrika kujadili masuala mbalimbali lakini mwaka 2017 rais Macron akizungumza jijini Ouagadougou nchini Burkina Faso alihidi kuwa nchi yake itachukua mfumo mpya wa kushirikiana na mataifa ya Afrika na haitoyaambia mataifa ya Afrika nini cha kufanya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.