Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Emmanuel Macron ajaribu kutuliza mvutano wa kidiplomasia na Algeria

Katika mahojiano yaliyorushwa Jumanne hii kulingana na kituo cha France 24, rais wa Ufaransa ameelezea nia yake ya kupunguza mvutano unaodhoofisha uhusiano kati ya Paris na Algiers, wakati Algeria imeamua kufunga anga yake kwa ndege za jeshi la Ufaransa na kumrejesha nyumbani balozi wake kufuatia kutangazwa kupunguzwa kwa visa vya Ufaransa kwa nchi hiyo ya Maghreb.

Rais wa Emmanuel Macron.
Rais wa Emmanuel Macron. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Wengi wanajiuliza ikiwa ni kumalizika kwa mvutano kati ya Paris na Algiers. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amependekeza, katika mahojiano yaliyorushwa Jumanne, Oktoba 5, kurejeshwa kwa uhusiano kati ya Paris na Algiers, wakati siku chache zilizopita kulishuhudiwa mvutano mkubwa wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Algeria.

"Matakwa yangu ni kwamba kuwe na utulivu kwa sababu nadhani ni bora kuzungumza kwa kila mmoja, ili kusonga mbele. Bila shaka kuna kutokubaliana lakini katika maisha, ni vema kuzunguma kinachowasibu na pia kuchangia matatizo hayo," amesema rais wa Ufaransa katika mahojiano ya Jumatatu jioni wiki hii aliyofanya na kituo cha France Inter na kurushwa leo Jumanne asubuhi.

"Hakika kutakuwa na mivutano mingine, lakini nadhani jukumu langu ni kujaribu kufanya kazi hii kuepuka hali kama hii isirudi kutokea", ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.