Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Mali: Macron ayataja maneno ya Waziri Mkuu wa Mali kama ya "aibu"

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ameelezea kushtushwa na kauli ya Waziri Mkuu wa Mali Choguel Maïga, kwenye Umoja wa Mataifa kuwa nchi ya Ufaransa imeiacha Mali, kauli ambayo amesema ni ya aibu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza baada ya chakula cha jioni katika ikulu ya Élysée, Septemba 30, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza baada ya chakula cha jioni katika ikulu ya Élysée, Septemba 30, 2021. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Maiga alielezea, mpango wa Ufaransa kupunguza vikosi vyake katika eneo la Sahel, vinavyoendelea na operesheni Barkhane, kukabiliana na majihadi kama, kuicha Mali.

Rais wa Ufaransa amesema maneno ya Waziri Mkuu wa mpito wa Mali Choguel Maïga hayakubaliki.

"Nakumbusha kwamba Waziri Mkuu wa Mali ni mmoja walioshirikishwa katika majaribio mawili ya mapinduzi, ninaweza kusema hivyo. Kwa kuwa kulikuwa na mapinduzi mwezi Agosti 2020 na ni mapinduzi ndani ya mapinduzi. kulingana na kanuni za kidemokrasia, serikali ya sasa si halali. Wakati jana tulitoa heshima zetu za mwisho kwa Sajenti Blasco na leo amezikwa, kile Waziri Mkuu wa Mali alisema hakikubaliki. Ni aibu. Na hiyo inadhalilidha hata serikali. "

Paris ililaani vikali katika siku za hivi karibuni matamshi yaliyotolewa Jumamosi na Choguel Maïga, ambaye alithibitisha kwamba tangazo la Emmanuel Macron mnamo mwezi Juni la kupitia upya uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali,  baada ya kumalizika kwa operesheni Barkhane, lilikuwa "aina ya kutelekezwa kwa Mali wakati bado inakabiliwa na changamoto za usalama ”.

"Najua sivyo raia wa Mali wanavyofikiria," amesema rais wa Ufaransa. Wamali ndio wahanga wa kwanza wa ugaidi wa kijihadi. Ninajua kuwa leo, Wamali wengi wanafikiria watoto wao waliouawa na magaidi hawa, lakini pia wanafikiria familia hizi za wanajeshi ambao walipoteza ndugu zaokwa kutoka kwao kwendau umbali wa maelfu ya kilomita kusaidia kuokoa Mali. Kuna dharau nyingi kutoka kwa uongozi wa sasa wa Mali kwa wanajeshi wetu, haikubaliki. "

Emmanuel Macron amesema hatarajii "chochote" kutoka kwa serikali ya Mali, kabla ya kuongeza kuwa serikali hiyo ingepaswa kuheshimu ahadi zake: kuandaa uchaguzi mwezi Februari na kuacha kuwaweka viongozi wa kisiasa gerezani.

Ninachotarajia ni kwamba mchakato wa uchaguzi ufanywe, kwamba wale ambao wapo madarakani kupitia jaribio la mapinduzi waheshimu demokrasia na kuacha kuwaweka jela viongozi wa kisiasa….

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.