Pata taarifa kuu
DRC

WHO yaomba radhi kwa madai ya ubakaji wa wafanyakazi wake DRC

Tume huru ya kuchunguza unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji uliofanywa na wafanyakazi wa shirika la Afya Duani, WHO, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebaini kwamba  wafanyakazi wa shirika hilo alijihusisha na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana nchini humo.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini, Kinshasa (DRC).
Siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini, Kinshasa (DRC). © MONUSCO/ Myriam Asmani
Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo inasema kuwa mfumo umeshindwa na uzembe wa mtu mmoja katika ripoti yake.

Kwa upande wake shirika la Afya Duniani limesema limesikitishwa na madai ya unyanyasaji wa ngono uliofanywa na wafanyakazi wake nchini DRC wakati wa mlipuko wa Ebola.

Shirika la afya duniani WHO limetaka uchunguzi ufanyika kuhusu shutuma kuwa wafanyakazi wa afya waliokuwa wakisaidia mapambano dhidi ya mlipuko wa Ebola nchini DRC waliwadhalilisha kingono na kuwanyanyasa wanawake.

Mkurugenzi wa WHO barani Afrika , Matshidiso Moeti ameomba radhi kwa wanawake na wasichana waliopata masaibu hayo kwa mwaka 2018 na 2020 kwasababu hatua kali zitachukuliwa kwa wafanyakazi hao na watumishi wengine wa afya.

Katibu mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema ripoti hiyo inafadhaisha kuisoma.

Vitendo hivyo vilifanyika mwaka 2018 na mwezi Machi mwaka 2020.

WHO na wafanyakazi wa mashirika mengine ya misaada walishutumiwa na wanawake 50 katika uchunguzi wa pamoja wa mashirika mawili ya habari.

Wanawake walipewa vinywaji, ''walivamiwa'' kwenye hospitali, wakishurutishwa kufanya ngono, na wanawake wawili wakapata ujauzito.

Shirika la habari linalotangaza masuala ya haki za binadamu na shirika la the Thomson Reuters yamefanya uchunguzi wa karibu mwaka mzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.