Pata taarifa kuu
AFRICA - COVID 19

WHO - Virusi vya Corona aina ya Delta vinaenea kwa kasi Africa

Shirika la afya duniani, WHO, limesema maambukizi ya virusi vya Corona aina ya delta yameanza kuenea kwa kasi barani Afrika, hali inayoliweka bara hilo katika hatari ya kushuhudia maafa makubwa wakati huu likikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Matshidiso Moeti, mkuu wa WHO barani Africa wakati alipotembelea mji wa Zuma, nchini Liberia
Aprili 22, 2015
Matshidiso Moeti, mkuu wa WHO barani Africa wakati alipotembelea mji wa Zuma, nchini Liberia Aprili 22, 2015 AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona imekuwa ikipanda kwa kipindi cha majuma sita yaliopita, watu alfu 202,000 wakiambikizwa kwa kipindi hicho.

Mataifa 3_ ya Africa kwa kipindi cho pia yamesajili vifo 3,000 ambavyo vimetokana na virusi vya corona aina ya delta.

Mkuu wa WHO barani africa, Matshidiso Moeti, anasema hali inayoshuhudiwa kwa sasa ni hatari na inahitaji juhudi za dharura kufanyika ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.

Virusi aina ya Delta vimeripotiwa kwa zaidi ya mataifa 16 barani Africa kufikia sasa, mataifa ya Uganda DRC yakiripotiwa kuathirika zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.