Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Zaidi ya wanafunzi 70 watekwa nyara kaskazini magharibi mwa Nigeria

Nchini Nigeria, wanafunzi 73 wa shule ya upili walitekwa nyara Jumatano wiki hii katika mji wa Kaya, katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Zamfara.

Moja ya darasa katika shule moja huko Jangebe, jimbo la Zamfara, ambapo wasichana 300 walitekwa nyara mapema mwaka wa 2021.
Moja ya darasa katika shule moja huko Jangebe, jimbo la Zamfara, ambapo wasichana 300 walitekwa nyara mapema mwaka wa 2021. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Huu ni mfululizo mrefu wa visa vya utekaji nyara ambavyo vimekumba sehemu hii ya Nigeria kwa miezi kadhaa. Kulingana na polisi, makundi ya majambazi yanachukulia ukatili huu wa utekaji nyara kama biashara muhimu.

Ilikuwa asubuhi ambapo "idadi kubwa ya majambazi wenye silaha walivamia" shule ya upili ya Kaya na kuwateka nyara wanafunzi 73, amesema msemaji wa polisi wa Zamfara katika taarifa.

Jumatano asubuhi shule za msingi na sekondari za serikali zilifungwa kwa muda na polisi inasema inafanya kiliochini ya uwezo wake kuhakikisha wanafunzi hao wanaachiliwa.

Kwa miezi kadhaa, visa vya utekaji nyara shuleni vimekuwa vikiongezeka katika majimbo ya kaskazini na kati ya nchi. Karibu wanafunzi 1,000 wametekwa nyara tangu kuanza kwa mwaka huu.

Wengi wao wameachiliwa kwa fidia, kama wanafunzi 18 wa shule ya kilimo huko Zamfara waliotekwa nyara katikati ya mwezi wa Agosti na kuachiliwa wiki iliyopita. Visa hivi vya utekaji nyara vinatekelezwa na makundi ya wahalifu, wanaojificha kwenye msitu wa Rugu kaskazini mwa nchi. Polisi inabaini kwamba makundi ya kigaidi yanayotekeleza uhalifu wao katika sehemu hii ya Nigeria kama Boko Haram, hayakusishwi katika visa hivyo kwa sasa, lakini hata hivyo inahofia kuwa kuna baadhiya makundi yanyohusiana na makundi hayo ya majambazi.

Ili kuzuia kuendelea kwa visa  hivyo, majimbo manne ya kaskazini magharibi yamechukua hatua kama vile kuweka muda wa kutembea kwa pikipiki, uuzaji wa mafuta, na kusitishwa kwa masoko na usafirishaji wa mifugo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.