Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Wanafunzi walioachiwa wakutanishwa na familia zao

Nchini Nigeria, Wanafunzi karibu 100 waliokuwa wametekwa na watu wenye silaha katika jimbo la Niger na baada kuachiwa, wamekutanishwa na wazazi wao baada ya miezi mitatu.

Wanafunzi sita wa Tegina walifariki wakiwa mikononi mwa watekaji nyara na wengine kumi na tano waliweza kutoroka mnamo mwezi Juni, kulingana na uongozi wa shule.
Wanafunzi sita wa Tegina walifariki wakiwa mikononi mwa watekaji nyara na wengine kumi na tano waliweza kutoroka mnamo mwezi Juni, kulingana na uongozi wa shule. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wengine 32 waliokuwa wametekwa kutoka Seminari ya Kiislamu wameachiwa, baada ya watu wenye silaha kulipwa fidia.

Mnamo Mei 30, karibu watu 200 wenye silaha za kivita walivamia mji wa Tegina, Jimbo la Niger (magharibi mwa Nigeria), na kuwateka nyara wanafunzi 136 kutoka shule ya kibinafsi ya Waislamu Salihu Tanko.

Tangu mwezi Desemba, Nigeria imekumbwa na mfululizo wa visa vya utekaji nyara  katika shule na vyuo vikuu.

Wanafunzi sita wa Tegina walifariki wakiwa mikononi mwa watekaji nyara na wengine kumi na tano waliweza kutoroka mnamo mwezi Juni, kulingana na uongozi wa shule.

Maeneo ya Kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria yanakabiliwa na ongezeko la mashambulio, uporaji na utekaji nyara, vitendo vinavyoendeshwa na magenge ya wahalifu wanaojulikana kijijini kama "majambazi". Lakini mwaka huu, magenge hayo yalianza kulenga wanafunzi kwa kwa kutarajia fidia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.