Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Sheria ya kutotoka nje yatangazwa katika Jimbo la Plateau

Serikali ya Jimbo la Plateau imetangaza sheria ya kutotoka nje ya masaa 24 katika eneo la Jos, baada ya sheria ya kutotoka nje ya saa 12 kutangazwa katika eneo la Jos Kaskazini na maeneo mengine mawili.

Jimbo la Plateau liko chini ya sheria ya kutotoka nje kwa saa 24 wakati mivutano ikiongezeka kati ya jamii za Wakristo na Waislamu.
Jimbo la Plateau liko chini ya sheria ya kutotoka nje kwa saa 24 wakati mivutano ikiongezeka kati ya jamii za Wakristo na Waislamu. © KOLA SULAIMON/AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi Agosti 14, msafara wa basi uliokuwa umebeba Waisalmu kutoka Jamii ya Wayoruba waliokuwa wanarejea kutoka katika muhadhara wa kidini ulishambuliwa. Watu 22 waliuawa na makumi kujeruhiwa.

Mvutano kati ya jamii unazidi kuongezeka kwani mashambulio na ulipizaji kisasi yamefuatana kwa wiki tatu mfululizo katika jimbo hilo.

Tangu Jumamosi na kutokana na vifo vya mahujaji wa Kiislamu waliouawa katika shambulio la msafara wao huko Jos, Gavana Simon Lalong amekuwa akitoa wito wa utulivu. amewaomba wakaazi wa Jimbo la Plateau kuepuka kitendo chochote au kauli ambayo inaweza kuchochea vurugu.

Uamuzi wa gavana kuweka Jos chini ya sheria ya kutotoka nje tangu Jumapili alasiri kwa saa 24 pia inaweza kuzidisha mvutano.

Katika taarifa yake ya Jumapili msemaji wa Jimbo la Plateau, Obah Ogaba alisema pamoja na kuwatia mbaroni watu kadhaa, amelitaja kundi la kabila la Irigwe kuhusika na mkasa huo.

Tukio hilo la mauaji linahisiwa kuwaa kulipiza kisasi na linadhaniwa limefanywa kwa bahati mbaya na kundi hilo la Irigwe, waliodhani watu waliowashambulia ni kutoka jamii nyingine ya Waislamu ya wafugaji ya Fulani.

Katika eneo la kusini mwa Nigeria kabila hilo Fulani la wafugani wanaohama hama limekuwa katika makabiliano makali ya kuwania ardhi na makabila mengine kadhaa kama Irigwe Yaruba na Igbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.