Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Wanafunzi 28 waachiliwa na watekaji nyara kaskazini magharibi mwa Nigeria

Kundi la wahalifu ambalo liliteka nyara vijana 121 katika shule ya upili kaskazini magharibi mwa Nigeria mapema mwezi Julaimwaka huu imewaachilia mateka wapya 28, lakini wanafunzi 87 wa shule ya msingi na sekondari bado wanashikiliwa.

"Ishirini na nane wameachiliwa na tumewakutanisha tena na wazazi wao," Mchungaji Joseph Hayab, mmoja wa viongozi wa Shule ya Upili ya Baptist  amesema.
"Ishirini na nane wameachiliwa na tumewakutanisha tena na wazazi wao," Mchungaji Joseph Hayab, mmoja wa viongozi wa Shule ya Upili ya Baptist amesema. © AP
Matangazo ya kibiashara

Julai 5, watue wenye silaha walivamia mabweni ya Shule ya Upili ya Bethel Baptist, iliyoko Chikun katika Jimbo la Kaduna, usiku, kabla ya kuwateka nyara wanafunzi wenye umri kati ya miaka 10 na 19.

 

Shambulio hili ni la hivi karibuni katika mfululizo wa utekaji nyara wa watoto na wanafunzi kaskazini magharibi mwa Nigeria na makundi ya wahalifu.

"Ishirini na nane wameachiliwa na tumewakutanisha tena na wazazi wao," Mchungaji Joseph Hayab, mmoja wa viongozi wa Shule ya Upili ya Baptist  amesema.

"Majambazi waliwaachilia jana na tukaenda kuwachukua na mabasi ya kanisa," ameongeza mchungaji huyo, ambaye amesema watoto walilala shuleni kabla ya viongozi kuwaita wazazi wao mapema Jumapili kuwaambia waje kuwachukua.

Polisi ya jimbo la Kaduna haijasema chochote kuhusiana na tukio hilo.

"Kwa jumla tuna watoto 34 ambao wamepata uhuru wao, na 87 ambao bado wanashikiliwa mateka na majambazi," mchungaji huyo amebaini.

- "Tunawaombea" watoto wengine -

Kwa kweli, "watoto watano walitoroka Julai 21, wawili kati yao walipatikana na polisi. Wengine watatu walifanikiwa kufika shuleni kwao," amesema Mchungaji Joseph Hayabji.

"Waliweza kutoroka wakati majambazi walipowatuma kuchukua kuni jikoni. Wiki mbili zilizopita, watekaji nyara pia walimwachilia mwanafunzi wa shule ya upili kwa sababu za kiafya," ameongeza.

Baada ya utekaji nyara, watekaji nyara walidai chakula na fidia kutoka kwa maafisa wa shule ili mateka waachiliwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.