Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Watu wanne wauawa katika shambulio mashariki mwa DRC

Angalau watu wanne waliuawa Jumatano wiki hii kwenye Barabara  kuu inayounganisha mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri, mikoa miwili inayoendelea kuwa chini ya sheria ya kijeshi.

Msafara wa magari ukisindikizwa na MONUSCO, Agosti 8, 2021.
Msafara wa magari ukisindikizwa na MONUSCO, Agosti 8, 2021. © Flickr / Monusco
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lililotekelezwa na waasi wanaoaminiwa kuwa wa ADF lililenga msafara uliokuwa ukisindikizwa na vikosi vya DRC na MONUSCO. Katika tukio hili, karibu magari kumi yalichomwa moto na watu kadhaa hawajulikani waliko.

Katika video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii, kunaonekana watu wakiangusha vilio na wengine wakifanya maombi kwenye gari ndogo, huku wengine mia kadhaa wakiwa katikati ya pande mbili ambako risasi zilikuwa zikirushwa.

Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Ofay, na Alhamisi hii asubuhi, iaddi ya vikosi vya usalama imeongezwa na doria imeshika kasi katika eneo hilo.

Kufuatia kuibuka tena kwa vurugu katika sehemu hii, jeshi la serikali na vikosi vya MONUSCO wamekuwa wakishindikiza misafara ya magari ya raia tangu Agosti 7. Ni hatua ya haraka ya kuzuia mashambulio dhidi ya raia wasio na hatia, kuhakikisha raia wanafanya shughuli zao kwa urahisi na kuwezesha wakaazi kufanya kazi, MONUSCO imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.