Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Kumi na tisa wauawa katika shambulio la ADF

Raia 19 wameuawa baada ya kushambuliwa na waasi wa Uganda wa ADF Wilayani Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Eringeti, eneo la Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo. Desemba 5, 2014: Mwanajeshi wa FARDC akitoa ulinzi.
Eringeti, eneo la Beni, Kivu Kaskazini, DR Congo. Desemba 5, 2014: Mwanajeshi wa FARDC akitoa ulinzi. MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema mauaji hayo yalitokea siku ya Ijumaa na baadhi ya miili kubainika siku ya Jumamosi, baada ya washukiwa wa ADF kuvamia kijiji cha Kasanzi.

Kiongozi wa kijiji hicho Kakule Kalunga, amesema watu hao 19 waliuawa kwa kuchomwa visu na wengine kupigwa risasi, huku nyumba zao zikichomwa moto.

Gavana wa zamani wa jimbo la Kivu Kaskazini Carly Nzanzu Kasivita kwenye ukrasa wake wa Twitter ameandika idadi ya vifo imeongezeka kutoka watu watano hadi 14 siku ya Jumamosi, huku nyumba 13 zikiteketezwa moto katika eneo la Rwenzori.

Meleki Mulala, kiongozi wa mashirika ya kiraia katika eneo la Rwenzori amesema ukosefu wa wanajeshi katika eneo hilo kumechangia pakubwa kutokea kwa mauaji hayo.

Tangu mwezi Mei, mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri imekuwa chini ya uongozi wa kijeshi, lakini mauaji ya raia yameendelea kuripotiwa na mauaji haya yamekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde kuzuru mikoa hiyo mwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.