Pata taarifa kuu
CAMEROON

Cameroon: maelfu ya watu wayatoroka makaazi yao kufuatia mapigano

Mapigano kati ya jamii mbili hasimu yamesababishavifo vya  watu 32 na 74 wamejeruhiwa katika eneo la Kaskazini mwa Cameroon, karibu na mpaka wa Chad.

Wavuvi katika eneo la Kaskazini mwa Cameroon.
Wavuvi katika eneo la Kaskazini mwa Cameroon. © 2ddanga/creative commons
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu wamekimbilia Chad na wengine ncini Cameroon kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) .

Watu 7,300 walikimbilia nchini Cameroon na wengine 11,000 waliingia nchini Chad, kulingana na mamlaka ya nchi hiyo: "85% ya watu ambao wamekimbilia upande wa Chad ni wanawake na watoto, wanaosalia ni wazee wanaume. Leo utulivu umerejea lakini hali bado ni ngumu kwa wakimbizi.

Chanzo cha vurugu hizi, ni mabishano kati ya wavuvi na wafugaji ambayo yaliongezeka wiki iliyopita. Agosti 10 katika eneo la Logone Birni, mvutano uligeuka kuwa mapigano katiya jamii mbili hasimu. Vijiji 19 vilichomwa moto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.