Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Côte d'Ivoire: Laurent Gbagbo kukutana na Alassane Ouattara katika ikulu ya rais

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara amemwalika mtangulizi wake Laurent Gbagbo kukutana naye katika ikulu ya rais tarehe 27 Julai mwaka huu.

Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo watakutana kwa mara ya kwanza Julai 27, 2021 tangu kumalizaka kwa machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2011.
Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara na mtangulizi wake Laurent Gbagbo watakutana kwa mara ya kwanza Julai 27, 2021 tangu kumalizaka kwa machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2011. AFP - ISSOUF SANOGO,SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Tangu kiongozi wa zamani wa nchi hiyo kurejea nchini mwezi uliopita baada ya kuachiliwa huru katika mahakama ya ICC, wengi wameendelea kusubiri mkutano huo wa kwanza kati ya wawili hao, mkutano ambao unatarajia kuashiria hatua muhimu kuelekea maridhiano ya kitaifa na kuboresha hali ya kisiasa.

Jumanne Julai 27 utafanyika mkutano wa kwanza kati ya Alassane Ouattara na Laurent Gbagbo tangu machafuko ya baada ya uchaguzi wa 2010-2011, ambao ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000 nchini Côte d'Ivoire kulingana na Umoja wa Mataifa. Itakuwa pia tarehe yao ya kwanza kukutana tangu kurudi kwa mpinzani huyo wa kihistoria mwezi uliopita.

Msemaji wa serikali Amadou Coulibaly, hata hivyo, amehakikisha kwamba rais anajaribu kkutana na wapinzani wake. "Kuna mazungumzo ambayo yalianza na Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly, ambayo yaliendelea na Waziri Mkuu Hamed Bakayoko na Waziri Mkuu Achi," amesema.

Mnakumbuka mikutano yote hapo ilikuwa ya kujiandaa kurudi kwa Laurent Gbagbo. Hakujawahi kuwa na usumbufu wowote katika mazungumzo katika nchi yetu na yataendelea kwa sababu hii ni nia ya mapenzi ya serikali ”.

Msemaji wa serikali ya Ivory Coast alitangaza hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Abidjan Jumatanowiki hii. Amadou Coulibaly alitangaza kuwa rais Alassane Ouattara atampokea Laurent Gbagbo Julai 27, Jumanne ya wiki ijayo, katika ikulu ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.