Gbagbo azuru DRC kumtembelea rafiki yake Jean-Pierre Bemba
Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo yupo nchini DRC kukutana na mwanasiasa wa upinzani Jean-Pierre Bemba na kuhudhuria sherehe ya harusi ya binti yake Bemba.
Imechapishwa:
Wawili hao walikutana kwenye Mahakama ya ICC walikoshtakiwa na kuwa marafiki wa dhati wakati wakikabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita.
Baada ya kuzuiwa kwa miaka 10 Gbagbo alirejea nchini mwake tarehe 17 mwezi Juni baada ya kufutiwa mashtaka na Mahakama ya ICC na hii ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi baada ya kurejea nyumbani.
Gbagbo hivi karibuni alidokeza kuwa alikuwa rafiki wa karibu wa Bemba baada ya pamoja kupatikana na makosa katika Mahakama hiyo ya Kimataufa lakini baadaye wakaachiwa huru baada ya kukata rufaa.