Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA

Laurent Gbagbo kurejea Cote d'Ivoire Juni 17

Rais wa zamani wa Cote d'Ivoire Laurent Gbagbo anatarajiwa kureja nyumbani Juni 17 mwaka huu baada ya kuachiliwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, mwezi Marichi.

Wafuasi wa Laurent Gbagbo na chama cha FPI wakiandamana huko Abidjan. (Picha ya kumbukumbu).
Wafuasi wa Laurent Gbagbo na chama cha FPI wakiandamana huko Abidjan. (Picha ya kumbukumbu). AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa kiongozi huyo wamekuwa wakimsubiri kwa hamu na gamu tangu pale alipoachiwa huru na mahakama ya ICC takriban miaka kumi tangu kuepelekwa, Hague, na sasa Laurent Gbagbo anajiandaa kurudi nchini mwake katika majuma mawili yajayo.

Laurent Gbagbo alisafishwa na mahakama ya ICC na baadae kuachiwa huru baada ya kutuhumiwaa mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, hatuwa inayoonekana kuwa ni ushindi wa kiongozi huyo dhidi ya  wapinzani wake wa kisiasa huko Côte d'Ivoire na nje ya nchi. Karibu wafuasi wake wote, waliokimbilia uhamishoni tangu mwaka 2011, wamerudi nchini Cote d'Ivoire.

Hata hivyo chama cha Laurent Gbagbo FPI kinasema kiongozi huyo harejei nchini kuja kulipiza kisase, bali anarudi kuwezesha maridhiano ambayo ni kiungo muhimu kilichokosekana, kulingana na chama hicho.

Hata hivyo huenda utata ukaibuka baadae juu ya namna chama cha kiongozi huyo wa zamani kinavyotaka kuandaa sherehe na mapokezi makubwa, wakati chama tawala nchini humo RHDP kinapinga hilo na kumtaka arejee kimya kimya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.