UN -Tatua swala la ubaguzi wa rangi duniani
Umoja wa mataifa umezitaka serikali kote duniani kumheshimu mmarekani mweusi George Floyd, aliyeuawa na polisi mzungu Derek Chauvin, mwaka uliopita nchini Marekani, kwa kutatua swala la ubaguzi wa rangi, katika mataifa yao.
Imechapishwa:
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya mauwaji ya Floyd, mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa, Michelle Bachelet, amesema njia pekee ya kumheshimu Floyd ni serikali katika mataifa yote duniani kutatua swala la ubaguzi wa rangi analosema linarejesha nyuma hatua zilizopingwa kwa dunia kuendelea.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa hali ya ubaguzi wa rangi duniani ni ya kutisha, na kwamba raia wengi wenye asili ya Kiafrica, hupitia mateso mikoni mwa maafisa wa usalama kote duniani.
Ripoti hiyo inasema raia wenye asili ya kiafrica hubaguliwa wakati wanapotafuta, ajira, nyumba na masomo na kushtumu serikali kwa kukosa kuangazia kwa kina swala hilo.