Pata taarifa kuu
MAURITANIA-UFISADI

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz akamatwa

Rais wa zamani wa Mauritania, Mohmamed Ould Abdel Aziz, alikamatwa siku ya Jumanne jioni mwendo wa saa nane usiku UT na kuwekwa kizuizini na jaji wa kitengo cha kupambana na ufisadi kutoka mahakama kuu ya Nouakchott-Ouest, mmoja wa mawakili wake ameviambia vyombo vya habari kwenye mji huo wa Nouakchott.

Rais wa zamani wa Mauritania Mohammed Ould Abdel Aziz
Rais wa zamani wa Mauritania Mohammed Ould Abdel Aziz © Ikulu ya Nouakchott, Mauritania
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye alilitawala taifa la Mauritania kati ya 2008 na 2019, mnamo mwezi machi 12 alishtakiwa kwa makosa ya ufisadi, ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi mabaya ya pesa za serikali, mashtaka ambayo hata hivyo amekuwa akiyakanusha.

Mkuu wa jopo la mawakili wake kiongozi huyo wa Mauritania wakili Mohameden Ould Ichidou, amelaani kitendo cha kukamatwa kwa rais Ould Abdel Aziz kwamba ni kinyume cha sheria na kaongeza kuwa mteja wake ameonewa.

Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari, mawakili wa kiongozi huyo wamechukulia kitendo hicho kuwa ni cha kisiasa na kwamba watahakikisha anaachiwa huru.

Mwezi Julai mwaka uliopita, kamati maalum iliyoundwa ili kuchunguza tuhuma za ubadhirifu na ufisadi zinazomkabili kiongozi huyo wa zamani wa Mauritania iliwasilisha ripoti yake, yenye kurasa 800 katika ofisi ya mwendesha mashtaka, ambapo rais wa zamani wa Mauritania, Mohmamed Ould Abdel Aziz alishitakiwa kwa makosa ya rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma, utapeli na matumizi mabaya ya mamlaka yake

Aziz alishtakiwa mnamo machi 12, mwaka wa 2021 kabla ya kuwekwa kizuizini nyumbani mnamo Mei 11, huku akiendelea kukanusha tuhuma zote dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.