Pata taarifa kuu
AFRIKA-UCHUMI

Mkutano wa kuokoa uchumi wa Afrika kufanyika Ufaransa

Karibu viongozi thelathini kutoka Afrika na Ulaya wanakutana Jumanne katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, na mashirika makubwa ya kimataifa ya kiuchumi, kwa mpango wa Ufaransa, kujaribu kuokoa uchumi wa Afrika inayotishiwa baada ya janga la COVID-19.

Noti za faranga za CFA.
Noti za faranga za CFA. AFP / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Afrika ni bara lililookolewa kwa suala la afya, likiwa na vifo 130,000 tu kutokana na COVID-19 kati ya jumla ya vifo karibu milioni 3.4 duniani kote. Lakini inakabiliwa na mdororo wa kiuchumi, licha ya kuepuka vifo vingi vinavyosababishwa na janga hilo.

Mkutano wa Paris ambao utaanza saa 7 mchana kwa saa za Ufaransa na Afrika ya Kati, chini ya uongozi wa Emmanuel Macron, utagawanywa katika vikao viwili, moja kuhusu suala la "ufadhili na kushughulikia deni la umma", na kikao kingine kuhusu "sekta binafsi barani Afrika ".

Rais wa Ufaransa Ufaransa Emmanuela Macron atahitimisha mkutano huo kwa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi, ambaye ni rais wa Umoja wa Afrika.

- Ukosefu wa ufadhili -

Wazo la "Mkutano huu juu ya Ufadhili wa Uchumi wa Afrika" uliibuka katika msimu wa joto 2020, wakati Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilipokadiri kwamba bara hilo liko hatarini kukumbwa na ukosefu mkubwa wa ufadhili wa dola bilioni 290, 'ifikapo mwaka 2023.

Ukuaji wa bara la Afrika, ambao uchumi wake ulishuka kwa mara ya wanza katika nusu karne mwaka jana kwa sababu ya janga hilo, unatarajiwa kuongezeka kwa 3.4% mnamo mwaka 2021 na 4% mnamo mwaka 2022.

Lakini hiyo haitatoshi. Madeni ya umma yanaiweka hatarini Afrika, kama umasikini: mnamo mwaka 2021, Waafrika milioni 39 wanaweza kukumbwa na umaskini uliokithiri, kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.