Pata taarifa kuu
CHAD

Chad kukumbwa na maandamano mapya

Upinzani na mashirika ya kiraia yanayopinga Baraza la Kijeshi la Mpito wametoa wito kwa maandamano mapya leo Jumatano. Wito wa kuingia mitaani unatolewa baada ya maandamano makubwa kushuhudiwa siku ya Jumanne katika viunga vya mji mkuu na katika miji mingine ya nchi hiyo.

Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye anaongoza Baraza la Jeshi la Mpito (CMT), alilihutubia taifa Jumanne Aprili 27 aakitoa wito kwa wananchi kuwa watulivu.
Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye anaongoza Baraza la Jeshi la Mpito (CMT), alilihutubia taifa Jumanne Aprili 27 aakitoa wito kwa wananchi kuwa watulivu. © Tele Tchad via AP
Matangazo ya kibiashara

Jana, makabiliano na vikosi vya usalama yalidumu masaa kadhaahuku watu watano wakiriopitwa kuuawa, kulingana na mamlaka, angalau tisa kulingana na mashirika ya kiraia. Pamoja na wengi waliojeruhiwa, na kukamatwa, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari.

Watu hao waliuawa wakishiriki maandamano yaliyopigwa marufuku na uongozi wa jeshi nchini humo, kupinga uongozi huo wa kijeshi.

Kiongozi wa serikali ya mpito Mahamat Idriss Déby alihutubia taifa baada ya machafuko hayo na kuwataka wananchi kuwa watulivu.

Naye rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameshtumu kushambuliwa kwa waandamanaji na wale wanaotaka kuingia madarakani kwa nguvu.

Nchi ya Chad imejikuta katika hali hii baada ya kifo cha aliyekuwa rais Idriss Deby karibu wiki moja iliyopita na nchi kukabidhiwa mwanae Mahamat idriss deby itno, ambaye anatarajiwa kuwa madarakani kwa miezi 18.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.