Pata taarifa kuu
CHAD

Chad: Waasi wa FACT wataka suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa sasa

Nchini Chad, siku moja baada ya mazishi ya Rais Idriss Déby, waasi wa kundi la FACT (Front for Alternation and Concord in Chad) wanasema wako tayari kusitisha mapigano na kushiriki kwenye meza ya mazungumzo.

Wanajeshi wa Chad wakiwa nyuma ya gari la kijesi aina ya Land Cruiser huko Koundoul, kilomita 25 kutoka mji wa Ndjamena, Januari 2020.
Wanajeshi wa Chad wakiwa nyuma ya gari la kijesi aina ya Land Cruiser huko Koundoul, kilomita 25 kutoka mji wa Ndjamena, Januari 2020. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Kundi al awaasi la FACT, Mahamat Mahadi Ali, anasema anataka, zaidi ya yowote, suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa sasa.

Tunakubali kusitisha mapigano, kwa suluhisho la kisiasa. […] Leo, lazima mazungumzo ya kitaifa yapewe nafasi, mazungumzo ambayo yatashirikishawanasiasa wote nchini Cahd bila kubaguwa.

Wakati huo huo Ummoja wa Afrika unataka utawala wa kijeshi uishe nchini Chad, huku jeshi likiwa na mgawanyiko.

Baraza la amani na usalama la Muungano wa Afrika lilielezea "hofu ya hatari kubwa " kuhusu jeshi kuchukua mamlaka na kumuweka madarakani Jenerali Mahamat Déby Itno uongozini na kuvunjwa kwa bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.