Pata taarifa kuu
CHAD

Chad: Deby aibuka mshindi wa uchaguzi wa rais

Rais wa Chad Idriss Deby ameshinda kwa kishindo uchaguzi wa urais, kulingana na matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais wa Aprili 11 yaliyotangzwa na Tume ya Uchaguzi.

Mshirika wa nchi za Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislam katika Afrika Magharibi na Kati, Idriss Deby ni mmoja wa viongozi wakongwe zaidi barani Afrika.
Mshirika wa nchi za Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislam katika Afrika Magharibi na Kati, Idriss Deby ni mmoja wa viongozi wakongwe zaidi barani Afrika. Ludovic MARIN POOL/AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Idriss Deby ameshinda kwa kura nyingi karibu katika maeneo yote, ispokuwa eneo moja kati ya maeneo 51 ambapo kura zimetangazwa kufikia sasa. Matokeo bado hayajatangazwa katika maeneo mengine 61.

Kilmapone Larme, anayehusika na masuala ya vifaa katika CENI, amesema bado hawajapata zaidi ya 30% ya matokeo ya uchaguzi.

Kundi la waasi lenye makao yake nchini Libya, Front for Alternation and Concord in Chad (FACT), lilishambulia kituo vikosi vya Chad kwenye mpaka wa nchi hiyo kaskazini mwa nchi siku ya uchaguzi.

Rais wa Chad, Idriss Deby Itno,akipiga kura huko Ndjamena, Aprili 11, 2021.
Rais wa Chad, Idriss Deby Itno,akipiga kura huko Ndjamena, Aprili 11, 2021. AFP - MARCO LONGARI

Waasi wa FACT walenga kuudhibiti mji mkuu N'Djamena

Siku ya Jumamosi, serikali ya Uingereza ilisema msafara wa FACT ulikuwa ukielekea kusini magharibi kuelekea mji mkuu N'Djamena na ulizidi mji wa Faya, kwenye umbali wa kilomita 770 (maili 478) na mji wa N'Djamena.

Msafara mwingine ulionekana ukikaribia mji wa Mao, karibu kilomita 220 kaskazini mwa N'Djamena, serikali ya Uingereza ilisema kwenye wavuti yake ya ushauri kwa kusafiri.

Urasibu wa Deby kuhusiana na utajiri wa mafuta wakosolewa

Mshirika wa nchi za Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa Kiislam katika Afrika Magharibi na Kati, Idriss Deby ni mmoja wa viongozi wakongwe zaidi barani Afrika, lakini dalili za kuongezeka kwa hasira zinajitokeza kuhusu usimamizi wake wa utajiri wa mafuta wa nchi hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Chad ililazimika kupunguza matumizi ya umma kwa sababu ya bei ndogo ya mafuta, bidhaa yake kuu ya inayoagizwa nje,hali  ambayo ilisababisha mgomo.

Viongozi wa upinzani walitoa wito kwa wafuasi wao kususia uchaguzi wa wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.