Pata taarifa kuu

Upinzani wadai Idriss Deby ameshinda kwa wizi

Kiongozi wa muda mrefu nchini Chad Saleh Kebzabo aliyewaambia wananchi wa taifa hilo kutoshiriki kwenye Uchaguzi wa urais, uliofanyika Jumapili iliyopita, amesema anaamini kuwa rais Idriss Deby hakuchaguliwa kwa muhula wa sita na wananchi wa taifa hilo

Kiongozi wa muda mrefu nchini Chad Saleh Kebzabo .
Kiongozi wa muda mrefu nchini Chad Saleh Kebzabo . DESIREY MINKOH AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kebzabo ambaye alionekana mpinzani mkuu wa Deby alijiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho kufuatia vitisho na kutoamini kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki.

“Tumepata tulichokitaka, wananchi wa Chad hawakupiga kura,na hawakumchagua Deby.Tunafahamu matokeo yalivyo na tunafahamu kuwa wanachii wa Chad walimkata. Miaka mitano iliyopita alipoteza uchaguzi lakini akafanya mapinduzi ya uchaguzi na kusalia madarakani na hilo atalifanya tena kuendelea kuwa madarakani, ninachokifahamu hatakuwa na amani hata akiendelea kutawala, ” amesema Saleh Kebzabo.

Baada ya zoezi la kuhesabu kura kumalizika, Tume ya Uchaguzi, inatarajiwa kumtangaza rais Deby ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30 kuendelea kuongoza nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.