Pata taarifa kuu
CHAD

Chad yafanya uchaguzi mkuu katika hali ya mvutano

Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa 6 asubuhi nchini Chad. Wagombea saba ndio wanashiriki kinyang'anyiro hicho, ikiwa ni pamoja na rais anaye maliza muda wake Idriss Déby - ambaye yuko madarakani kwa zaidi ya miaka 30 - na ambaye anatafuta muhula wa 6.

Zoezi la kupiga kura katika mitaa ya Ndjamena, wakati wa uchaguzi wa mwezi Aprili 2016.
Zoezi la kupiga kura katika mitaa ya Ndjamena, wakati wa uchaguzi wa mwezi Aprili 2016. © AFP/Issouf Sanogo
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya vyama vya upinzani vimejiondoa kwenye kinyang'anyiro hiki na kutoa wito kwa raia kususia uchaguzi huo ili kulaani vurugu dhidi ya upinzani. Moja ya changamoto za siku ya leo itakuwa ni ushiriki.

Katika mitaa ya mji mkuu, uchaguzi huo umezua hisia tofauti: "Sitapiga kura," amesema mfanyabiashara mmoja katika soko kuu. "Hakuna upinzani wa kweli," ameongeza.

Wagombea watatu wa upinzani walijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho mwezi uliopita - pamoja na mpinzani wa kihistoria wa rais Deby Saleh Kebzabo ... ambaye ametoa wito kwa raia kususia uchaguzi huo. Wito ambaoumeungwa mkono na mkosoaji mwingine mkubwa wa rais Deby, Succès Masra. Mwanasiasa huyu alikataliwa kuwania katika uchaguzi huu kwa sababu bado ni mchanga sana kuweza kugombea. Lakini aliweza kuhamasisha sehemu kubwa ya vijana ambao wamekuwa wakijaribu kuandamana kila Jumamosi dhidi ya muhula wa 6 wa rais Déby.

Vyama kadhaa kadhaa vya kiraia, pamoja na mashirika ya haki za binadamu, pia yameitikia wito wa kususia uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.