Pata taarifa kuu
UCHUMI

TOTAL na CNOOC kujenga bomba la mafuta ghafi Hoima-Tanga

Viongozi wa Uganda na Tanzania wamesaini mikataba ya ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima mpaka bandari ya Tanga.

Rais Museveni n Irene Muloni, Waziri wa Nishati na Madini, wakati wa kuweka jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima mpaka bandari ya Tanga.Hoima-Tanga, le 11 novembre 2017.
Rais Museveni n Irene Muloni, Waziri wa Nishati na Madini, wakati wa kuweka jiwe la msingi la kuanza kwa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima mpaka bandari ya Tanga.Hoima-Tanga, le 11 novembre 2017. RFI/Grilhot
Matangazo ya kibiashara

Bomba hilo linatarajiwa kuwa na urefu wa zaidi ya Kilomita 1,’400 linagharimu Dola za Marekani Bilioni 3.5 na linatarajiwa kuwa refu zaidi duniani.

Kampuni ya mafuta kutoka Ufaransa Total na CNOOC kutoka China, zimekabidhiwa kazi ya kujenga bomba hilo ambalo linatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Ujenzi huo utagharimu dola za Marekani bilioni 3.55, na unatarajiwa kuwa mradi wenye bomba refu zaidi la mafuta duniani.

Uganda inakadiriwa kutoa mapipa yake ya kwanza ya wastani wa bilioni 1. 4 ya mafuta yanayofaa kibiashara mnamo 2025.

 Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa katika ziara ya Kwanza nje ya nchi yake, tangu kukabidhiwa madaraka mwezi uliopita, naye amesema mradi huo utasaidia kuimarisha uchumi wa mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.