Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UN

UN yakubali ombi la Ethiopia kuhusu uchunguzi Tigray

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amekubali ombi kutoka Ethiopia kuanzisha uchunguzi wa pamoja katika jimbo la Tigray, kaskazini mwa nchi, ambapo Bachelet anaamini kuwa uhalifu wa kivita unaweza kuwa umefanywa.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet.
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet. Juan Carlos Ulate/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi huko Tigray yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamia ya maelfu kuyatoroka makaazi yao.

Awali Umoja wa Mataifa ulielezea wasiwasi wake juu ya ukatili uliofanywa huko Tigray, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akilaani mauaji ya kikabila.

Michelle Bachelet "amejibu vyema" ombi kutoka kwa Tume ya Haki za Binadamu ya Ethiopia (EHRC) - taasisi ya umma - kwa kuanzishwa uchunguzi wa pamoja huko Tigray, msemaji wake Jonathan Fowler amesema.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa na EHRC zinaandaa "mpango wa uchunguzi, ambao unajumuisha mambo muhimu na mipangilio ya kiutendaji, ili kuzindua uchunguzi huu haraka iwezekanavyo", ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.