Pata taarifa kuu
MAREKANI-ETHIOPIA

Marekani yalaani mauaji ya raia katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amelaani mauaji ya kikabila katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, yanayodaiwa kutekelezwa na vikosi vya nchi ya Eritrea na vya nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani  Antony Blinken, akiwa Ofisini kwake Machi  3, 2021.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken, akiwa Ofisini kwake Machi 3, 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Blinken  akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Mambo ya nje katika bunge la Seneti nchini Marekani, ametaka kuondoka mara moja kwa vikosi hivyo na uchuguzi huru kufanyika kubaini kilichofanyika katika jimbo hilo, na kuwepo kwa kikosi kipya ambacho kitawalinda raia.

Kuna wanajeshi kutoka Eritrea na wengine kutoka jimbo jirani la Amhara.Wanastahili kuondoka na kuruhusu jeshi ambalo litaheshimu haki za watu wa jimbo la Tigray na kuacha mauaji ya kikabila ambayo tumeshuhudia Magharibi mwa jimbo la Tigray.

Aidha, ametaka uchunguzi huru kufanyika katika jimbo hilo kuhusu mauaji na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyoripotiwa.

Ethioipia na Eritrea kwa nyakati tofauti, zimekanusha wanajeshi wao kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji na mateso ya raia katika jimbo hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.