Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-UN-USALAMA

Wanajeshi wa Etiopia na Eritrea wahusishwa katika uhalifu Tigray

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za biandamu inasema uchunguzi wao umebaini kuwa, wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea wametekeleza uhalifu wa kivita na binadamu dhidi ya wakaazi wa jimbo la Tigray.

Wakazi wa kijiji cha Tigray cha Dengolat wanasema wanajeshi wa Eritrea waliwaua wanaume na wavulana siku moja baada ya sikukuu takatifu.
Wakazi wa kijiji cha Tigray cha Dengolat wanasema wanajeshi wa Eritrea waliwaua wanaume na wavulana siku moja baada ya sikukuu takatifu. EDUARDO SOTERAS AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume hiyo Michelle Bachelet katika taarifa yake amesema kuwa, kutokana na hali hiyo, kuna umuhimu wa kufanyika kwa uchunguzi huru kuangazia kinachoendelea katika jimbo la Tigray.

Aidha, amesema kuwa Ofisi yake ilipata habari ya matukio ya wanajeshi wa Ethioipia na Eritrea waliokuwa wanashambulia miji ya Mekelle, Humera na Adigrat kwa silaha nzito mwezi Novemba mwaka uliopita.

Wanajeshi wa Eritrea wamedaiwa kutekeleza ukiukwaji mkunbwa wa haki za binadamu ikiwa ni pamloja na kutekeleza mauaji katika Γͺneo la Axum katika ya Jimnbo la Tigray.

Pamoja na majeshi ya nchi hizo mbili, vikosi vya wapiganaji katika jimbo hilo la Tigray na lile kutoka jimbo la Amhara, yanatuhumliwa pia kuhusika, wakati huu vita vikiendelea kuripotiwa katika maeneo ya jimbo hilo.

Mataifa hayo mawili, yamekanusha kuwepo kwa vikosi vya Eritrea katika jimbo hilo ambalo bado lina uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.