Pata taarifa kuu
NIGERIA

Kisa cha utekaji nyara cha watu 42 chaibua hasira miangoni mwa raia wa Kagara

Watu wasiojulikana wenye silaha waliendesha shambulio dhidi ya shule ya sekondari katika jimbo la Niger, nchini, Nigeria usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki hii, na kuwateka nyara wanafunzi kadhaa, msemaji wa gavana wa jimbo hilo amesema.

Magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria
Magaidi wa Boko Haram nchini Nigeria REUTERS/Zanah Mustapha
Matangazo ya kibiashara

Washambuliaji walivamia shule ya bweni katika chuo cha serikali huko Kagara karibu saa nane usiku, na kudhibiti idara ya usalama ya shule hiyo, wakaazi wamesema.

Washambuliaji hao waliua mwanafunzi mmoja na kuwateka nyara wengine 27, waalimu 3, na raia , wakaazi 12 wa eno hilo la Kagara. Tukio hili jipya limeibua hasira miongoni mwa raia nchini Nigeria.

Msemaji wa gavana wa jimbo la Niger amethibitisha kwamba wanafunzi wengi wametekwa nyara, bila kutaja idadi ya wanafunzi hao.

Watu waliohusika na shambulio hili bado hawajajulikana.

Kundi la wanamgambo wa Kiislam la Boko Haram na tawi la kundi la Islamic State wanaendesha harakati zao Kaskazini mwa Nigeria, lakini visa vya utekaji nyara na makundi mengine yenye silaha - hasa yakiomba fidia  pia vimekuwa vikiripotiwa katika eneo hilo.

Msemaji wa shirika la kimataifa la haki za Binadamu la Amnesty International amesema amezungumza na wazazi wa wanafunzi huko Kagara, ambao wamethibitisha shambulio hilo.

Idadi kubwa ya vikosi vya usalama vimetumwa katika eneo hilo na rais Muhammadu Buhari ameagiza vikosi vya usalama kuwarudisha mateka wakiwa 'salama'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.