Pata taarifa kuu
UMOJA WA AFRIKA

Moussa Faki Mahamat kuwania kwenye nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya AU bila mshindani dhidi yake

 Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali kutoka barani Afrika utafanyika katika muda wa wiki moja huko Addis Ababa, katika makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Moussa Faki Mahamat, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika
Moussa Faki Mahamat, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika RFI/Paulina Zidi
Matangazo ya kibiashara

Kwenye ajenda ya mkutano huo, rais wa DRC Félix Tshisekedi atakuwa rais wa sasa wa umoja huo. Lakini viongozi wengi barani Afrika wamejikita katika uchaguzi wa rais mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Nafasi ambayo mwenyekiti anayemaliza muda wake Moussa Faki Mahamat ndiye mgombea pekee katika kinyang'anyiro hiki. Lakini mchezo bado haujamalizika kabisa.

Wakuu wa nchi na serikali hawatafanya safari kwenda Addis Ababa, kwa sababu ya janga la Corona. Kwa hiyo itakuwa mkutano wa kilele kwa njia ya video. Tkio jingine lisilo la kawaida ni kwamba wakuu wa nchi watazingatia hasa utamaduni.

Pia kwenye ajenda ya mkutano huo, janga la COVID-19 na majibu ya Umoja wa Afrika kwa janga hili. Maswala ya amani na usalama ambayo kawaida huchukua muda mrefu katika mikutano kama huo hayako kwenye ajenda ya mkutano huu.

Lakini suala kubwa la mkutano huu ni uchaguzi wa mwenyekiti  mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika, ambaye atapitishwa kwa theluthi mbili ya nchi Wanachama 55.

Moussa Faki, ambaye ameshikilia wadhifa huo kwa miaka minne, ni kwa mara ya kwanza katika historia, kuwania nafasi hiyo bila mshindani yeyote dhidi yake.

Raia huyo wa Chad anaungwa mkono na nchi zinazozungumza Kifaransa, kulingana na washirika wake wa karibu. Hii sivyo ilivyo kwa nchi za kusini mwa Afrika, ambazo zinamshutumu kwa "kutowajibika" kwa kazi yake. Ikiwa haitapata kura zinazohitajika, Umoja wa Afrika utafungua njia kwa wagombea wengine.

Moussa Faki na timu yake wataendelea na majukumu yao, kabla ya mkutano mpya baada ya kipindi cha miezi sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.