Pata taarifa kuu
MISRI

Mali za rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi zazuiwa

Mahakama nchini Misri imezuia mali ya rais wa zamani wa nchi hiyo Mohammed Morsi na wanachama wengi 88 wa kundi la Muslim Brotherhood.

Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi akiwa Mahakamani siku zake akiwa hai
Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi akiwa Mahakamani siku zake akiwa hai REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Morsi alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo, aliaga dunia mwezi Juni mwaka 2019 akiendelea na kesi ya mashtaka dhidi yake baada ya kuwa gerezani kwa miaka Sita.

Alipinduliwa kijeshi na rais wa sasa, jenerali mstaafu Abdel-Fattah el-Sissi baada ya kuwa madarakani kwa mwaka mmoja, kutokana na misiruru ya maandamano mwaka 2013.

Aliondolewa na kushikiliwa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja baadae baada ya kufanyika maandamano makubwa kupinga utawala wake.

Baada ya kuondolewa madarakani, mamlaka zilipambana na wafuasi wake na wapinzani wengine, na kukamata maelfu ya watu.

Muslima Brotherhood na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, mshirika wa karibu wa Morsi ni miongoni mwa walioshutumu utawala wa Misri kuhusu kifo cha Morsi.

Rais wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi alizikwa saa chache baada ya kufariki dunia akiwa mahakamani.

Wakati huo makundi ya watetezi wa haki za binaadamu, ambayo yalikosoa mazingira ambayo Morsi aliwekwa kizuizini, walitoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu kifo chake.

Mohammed Morsi alizaliwa katika kijiji cha El-Awwadh katika jimbo lililopo kwenye delta za mto Nile la Sharqiya mwaka 1951.

Alisomea Uhandisi katika chuo Kikuu cha Cairo katika miaka ya 70 kabla ya kuhamia nchini Marekani ambapo alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Uhandisi.

Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru mwaka 2012, akiwa kiongozi mwandamizi wa kundi la kiislamu la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku kwa sasa nchini humo.

Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano ya wanaharakati ambao walimshutumu yeye na kundi la Muslim Brotherhood kujilimbikizia madaraka.

Baada ya maandamano kuwa makubwa, na wafuasi wa Morsi kushambulia wapinzani wake, jeshi likiwa chini ya rais wa sasa Abdel Fattah el-Sisi liliendesha mapinduzi na kumng'oa Morsi madarakani, Juni 2013.

Jeshi liliendelea kupambana na wafuasi wa Morsi baada ya mapinduzi, na zaidi ya wafuasi wake 1,000 waliuawa Agosti 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.