Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-USHIRIKIANO

Jean-Yves Le Drian nchini Mali, ziara ya kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian anazuru Mali leo Jumapili kwa ziara ya siku mbili. Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa kiraia wa Ufaransa tangu mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 18.

Waziri wa Mambo ya nje, Jean-Yves Le Drian.
Waziri wa Mambo ya nje, Jean-Yves Le Drian. SAFIN HAMED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa atakuwa na mazungumzo hasa na rais wa mpito na Waziri wake Mkuu Moctar Ouane. Paris inataka kujadili kuhusu amani na usalama, lakini pia kutoa msaada wake kwa taasisi za mpito.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa anakwenda nchini Mali kudhibitisha nia ya nchi yake ya kuunga mkono mabadiliko ya kisiasa na kusaidi taasisi za mpito. Katika muktadha huu, wakati wa ziara yake, Jean-Yves Le Drian atasaini mikataba kadhaa ya ushirikiano, katika sekta ya kusambaza maji safi kwa raia au kusaidia kuwawezesha wanawake.

Lakini kwa kufanya ziara hii, Waziri Le Drian anataka kutuma ujumbe: kama washirika wengine, Paris inaendelea kuwa makini kuhusu kipindi cha mpito, miezi kumi na nane, na uheshimishwaji wa ahadi zilizotolewa na nchi ya Mali kwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS). Wakati wa kipindi cha mpito, hatuwezi kufanya kila jambo, lazima yale yanayotakiwa kupewa kipaumbele, hasa kuweka mazingira bora katika kuandaa uchaguzi wa wazi.

Jean-Yves Le Drian atakuwa na mazungumzo na rais wa mpito, Bah Ndaw, na makamu wa rais (ikiwa atakuwa amerudi kutoka mikoani) na Waziri Mkuu Moctar Ouane. Amani na usalama katika nchini Mali pia vitakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo.

Ufaransa ina zaidi ya wanajeshi 5,000 nchini Mali na nchi zingine za Saheli kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.