Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: Wanasiasa wa Mali wawataka raia kuamua juu ya hatima ya nchi yao

Wakuu wa mataifa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, ambao wamehitimisha mkutano wao wa pili katika siku zisizozidi kumi, wameamua kuendeleza vikwazo dhidi ya Mali.

Watu wakikusanyika karibu na eneo la Uhuru huko Bamako, Agosti 19, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Watu wakikusanyika karibu na eneo la Uhuru huko Bamako, Agosti 19, 2020 (picha ya kumbukumbu). AP Photo/Atouna Sissoko
Matangazo ya kibiashara

Vingozi wa ECOWAS wameendelea kusisitiza juu ya uwepo wa serikali ya kiraia, baada ya jeshi kuhudumu kwa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja.

Viongozi wa ECOWAS wamebaini kwamba vikwazo hivyo vitaondolewa iwapo jeshi litakubali kurejesha utawala wa kiraia, baada ya kuhudumu kwa kipindi cha mpito cha miezi kumi na mbili.

Wakati huo huo wanasiasa nchini Mali wamewataka raia wa nchi hiyo kuamua juu ya hatma ya nchi yao.

Kipindi chote jeshi litakuwa madarakani, shinikizo kutoka kwa wakuu wa nchi za ECOWAS litaendelea kuikabili nchi ya Mali.

"ECOWAS yenyewe inatambua kuwa leo katika kanda nzima, kuna mgogoro mbaya wa kiusalama, kiafya, na kiuchumi. Kwa nini wakubali kuitumbukiza Mali katika mgogoro mkubwa zaidi wakati wasikiliza suluhisho kutoka makundi mbalimbali wanaweza kuisaidia nchi hii kuondokana na mgogoro unaoikabili", amesema Mountaga Tall, mmoja wa wanaharakati wa vuguvugu lililoanzishwa Juni 5 dhidi ya utawala wa Ibrahim Boubacara Keita.

Kwa upande aw ECOWAS, dharura ni uundwaji wa serikali ya mpito ya kiraia. Waziri Mkuu wa zamani Moussa Mara anakubaliana na hoja hii. "Ni kwa raia wa Mali kutoka fikra ya kuepo na utawala wa kiraia ili nchi iendelea kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kiuchumli ya Nchi za Afrika ya Magharibi, ECOWAS, " amesema Moussa Mara.

Uongozi wa kijeshi unatarajia kukutana na mashirika ya kiraia na vyama vya kisiasa katika mkutano ambao unasubiriwa kwa hamu na raia wengi wa Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.