Pata taarifa kuu
MALI-IBK-SIASA-USALAMA

Mali: Aliye kuwa rais wa Mali IBK aachiliwa huru

Aliye kuwa rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, aliyekamatwa Agosti 18 na kundi la wanajeshi lililofanya mapinduzi, ameachiliwa huru leo Alhamisi, jeshi limetangaza. Duru za kuaminika zinabaini kwamba mwanae, Karim Keita, alifaulu kuondoka nchini na kwa sasa yuko ukimbizini nje ya nchi.

Aliye kuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (picha ya kumbukumbu).
Aliye kuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (picha ya kumbukumbu). Photo: Issouf Sanogo/AFP
Matangazo ya kibiashara

Baraza kuu la kitaifa, lililoowekwa na wanajeshi kuiongoza nchi, "linaarifu wananchi wa Mali na jumuiya ya kimataifa kwamba aliye kuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta ameachiliwa huru na kwa sasa yuko nyumbani kwake", CNSP imetangaza kwenye mtandao wa Facebook.

Aliye kuwa rais wa Mali yuko huru na anaweza kufanya shughuli zake na kutembea anapotaka. Kwa sasayuko nyumbani kwake kwa mujibu wa afisa mmoja wa kundi hilo la wanajeshi.

Mmoja kati ya ndugu zake, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema IBK alirejea nyumbani kwake katika eneo la Sebenikoro wakati wa usiku.

Duru za kuaminika zimebaini kwamba Karim Keïta, mwanae IBK, alifaulu kuondoka nchini Mali. Habari hiyo imethibitishwa na chanzo kilicho karibu na familia yake na vyanzo vya usalama.

Karim Keïta, picha iliyopigwa Julai 11, 2018 huko Bamako.
Karim Keïta, picha iliyopigwa Julai 11, 2018 huko Bamako. Michele CATTANI / AFP

Karim Keïta, 41, ni mwanasiasa nchini Mali na mfanyabiashara. Alikuwa mjumbe katika bunge la kitaifa tangu mwaka 2013. Ana ungwa mkono na watu wengi nchini Mali, lakini pia ana wapinzani katika kisiasa na katika sekta ya uchumi nchini humo.

Katika wiki chache zilizopita kabla ya mapinduzi, alikuwa amestaafu kidogo baada ya kujiuzulu kwenye nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya Ulinzi ya Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.