Pata taarifa kuu
DUNIA-UISLAMU-SALA-JAMII

Waislamu washerehekea sikukuu ya Eid al-Adha

Waislamu katika maeneo mbalimbali duniani wanasherehekea kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu wiki ijayo siku kuu ya Eid al-Adha katika kiwingu cha Corona.

Maandalizi ya sherehe ya siku kuu ya Eid al-Adha yametatizwa mwaka huu na virusi vya Corona (picha ya kumbukumbu)
Maandalizi ya sherehe ya siku kuu ya Eid al-Adha yametatizwa mwaka huu na virusi vya Corona (picha ya kumbukumbu) AFP/Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Karibu watu milioni 2.5 huelekea miji mitakatifu ya Makka a na Madina kila mwaka kwa ibada ya kuhiji. Lakini kwa sababu ya virusi vya Corona, Saudi Arabia imepiga marufuku wageni kutoka nchi za nje kuingia nchini humo na kuruhusu idadi ndogo tu ya wenyeji kushiriki kwenye ibada hiyo.

Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara/kuchinja"

Waislamu hutumia Eid ul-Adha kusherehekea utiifu kamili wa nabii Ibrahimu kwa amri ya Mungu na kuwakumbusha wenyewe kuwa tayari kutoa kafara chochote ili kutimiza maagizo ya Mungu na kumfuata.

Kulingana na sheria za Kiislamu, Mwenyezi Mungu alimweka katika jaribio Nabii Ibrahim ili kutambua utiifu wake kwake kwa kumuagiza kumtoa sadaka mwanawe wa kiume na wa kipekee, Ismael. Utiifu wa Ibrahim na mwanawe ulizawadiwa na Mungu kwa kumwacha hai Ismael na badala yake kumteremshia kondoo, kisha kumjaalia mtoto mwingine kwa jina Is-haq.

Kwa kukamilisha hajj mtu huwa ametimiza nguzo ya tano ya Uislamu ambapo kila muislamu mwenye uwezo hutakiwa kuitimiza alau mara moja maishani mwake.

Ibada ya Hija kwenda Makka huanza siku mbili kabla ya Eid al-Adha na tarehe yake huthibitishwa baada ya kuoenakana kwa mwezi huo wa Dhu al-Hija.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.