Pata taarifa kuu
DRC-CORONA-UCHUMI

DRC: Tshisekedi atangaza mpango ghali wa kupambana na mdororo wa uchumi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Félix Tshisekedi, amesema kuwa anazidi kuwa na wasiwasi kutokana na mdororo wa uchumi unaosababishwa na janga la Corona.

Rais Tshisekedi Novemba 15, 2019.
Rais Tshisekedi Novemba 15, 2019. Photo: Tobias schwarz/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hiyo rais Tshisekedi amezindua "mpango wa dharura" wenye thamani ya Dola Milioni 2;6 unaolenga kupunguza athari za janga la Corona.

Kwa kuzindua mpango huu mpya wa ufadhili, rais Tshisekedi anajaribu kuinua uchumi wa nchi yake, lakini bado hali ni nzito: "Ahadi zetu ni kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi na ustawi wa raia umedorora, na hii inavuruga wazi mafanikio kwa matarajio yetu, 3 amesema rais aw DRC.

Mpango wa serikali unajikita katika mambo matatu: kuzuia na kudhibiti magonjwa hatari ya kuambukia, kuiimarisha na kusaidia kuinua uchumi. Ili kufanikisha yote hayo, serikali inapanga kutumia kiwango cha chini cha dola milioni 50 kwa mpango huo kwa kila mwezi. Fedha ambazo zitatoka kwenye mapato madogo ya serikali katika nyakati hizi ambapo karibu sekta zote zinakabilia na hali ya sintofahamu.

Serikali inategemea hasa kwenye sekta ya madini, ambayo hata yenyewe tayari imeathirika.

Zaidi ya dola bilioni 1.8 zinabaki kujazwa. Lakini, kwa upande wa wafadhili, waliomba kuepo na programu maalum, na hatua dhidi ya athari hizo ili kuhakikisha ufanisi wa mpango huo. Tayari Benki ya Dunia na shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, wameahidi kuipa serikali ya DRC mkopo na msaada wa zaidi ya Dola Bilioni 2 tangu mwezi Desemba kwa minajili ya kutekeleza miradi mbalimbali.Taasisi zote hizi mbili za fedha zinahitaji utawala bora ili fedha hizo ziweze kutolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.