Pata taarifa kuu
DRC-BENI-LUCHA-USALAMA

DRC: LUCHA yakaribisha hatua ya kusimamishwa kazi mea wa mji wa Beni

Vuguvugu kwa ajili ya mabadiliko nchini DRC, LUCHA, limesema limefurahishwa na uamuzi wa kusimamishwa kazi kwa mea wa Beni, Buanakawa Masumbuko Nyoni, kupitia agizo la Gavana wa mkoa wa Kivu kaskazini Carly Kasita, kwa tuhuma ya kutenda na kutamka maneno yaliyo kinyume na utaratibu wa afisa wa serkali.

Wanaharakati wa vuguvugu la LUCHA wakiandamana katika soko la Virunga huko Goma mwaka 2018.
Wanaharakati wa vuguvugu la LUCHA wakiandamana katika soko la Virunga huko Goma mwaka 2018. PATRICK MEINHARDT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Buanakawa Masumbuko Nyoni madiwani alisikika kwenye radio moja jijini Beni akiwashtumu wabunge na serkali ya mkoa wa Kivu Kaskazini kuwa ndio chanzo cha ukosefu wa usalama katika mji wa Beni.

"Leo tunashukuru na tuna furaha kubwa kuona mea ameweza kuwekwa kando lakini haitoshi kwetu sisi ,tunasubiri waweze kumfuta kazi, na mahakama iweza kufwatilia wale ambao walihusika kwa mauaji ya Freddy Marcus kambale mmoja wetu wa LUCHA, " amesema Esai Liko, mmoja wa wanaharakati wa LUCHA.

Jiji na wilaya ya Beni vya endelea kushuhudia mauaji yanayotekelezwa na waasi wa ADF kulingana na serikali ya DRC na zaidi ya watu 600 wameuawa tangu mwezi Oktoba 2019 pale jeshi la DRC lilipoanzisha operesheni kabambe dhidi ya waasi wa Uganda wa ADF.

Watu wanaovalia sare za vikosi vya usalama na ulizi wameonekana wakiwatishia usalama raia wasiokuwa na hatia katikati mwa jiji, wakala msambazaji wa vocha kupitia simu za mkononi na watu wengine wawili waliuawa jioni. Na, katika maandamano ya amani yaliyoandaliwa na shirika la kiraia la Lucha kwa kulaani ukosefu huu wa usalama, Billy Kambale, mwanaharakati ambaye alikuwa bado kijana, aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi mchana kweupe. Maandamano ya raia yaligeuka na kumtaka meya wa mji aw Beni kujiuzulu.

Mbale, mkazi wa Beni, amesema meya wa mji wa Beni hakuwajibika kwa kazi yake. Ambebaini kwamba, baada ya kuwa kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka kumi, imeonekaa kuwa kazi ya Buanakawa Nyonyi haikuwa nzuri .

Kwa upande wake Buanakawa Nyonyi, amesema maamdamano hayo yaliandaliwa ili kumpaka tope kwa lengo la kumtimuwa kwenye wadhifa wake.

Katika agizo la kusimamishwa kazi, gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini alibaini kwamba meya wa mji wa Beni alishindwa kujizuia katika taarifa zake, vile vile na "vitendo vya kupindukia" na kuweka hatarini mamlaka ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.