Pata taarifa kuu
DRC-ZAMBIA-UHASAMA-USALAMA

Mzozo kati ya DRC na Zambia: Kinshasa yakubali Brazzaville kuwa mpatanishi

Waziri wa Mambo ya nje wa Congo-Brazzaville alipokelewa Alhamisi Mei 28 na rais wa DRC Félix Tshisekedi. Jean-Claude Gakosso amekuwa ameleta ujumbe kutoka kwa rais Denis Sassou-Nguesso kwa mwenzake wa DRC.

RAis wa Congo-Brazzaville Denis Sassou-Nguesso.
RAis wa Congo-Brazzaville Denis Sassou-Nguesso. EVGENIA NOVOZHENINA / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya wawili hao yalifanyika katika eneo la Umoja wa Afrika, kwenye milima ya Mont-Ngaliema. Rais wa DRC amesema anathamini mchakato uliyoanzishwa na mwenzake wa Congo-Brazzaville, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, ICGLR.

Denis Sassou-Nguesso anatarajia, katika siku chache zijazo, kuanzisha mazungumzo yatakayozileta pamoja nchi nne, ikiwa ni pamoja na DRC na Zambia, nchi ambazo hivi karibuni zimeingia katika mzozo wa mpaka.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa pia ataalikwa kwenye mkutano huu kwa niaba ya Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.

Na ni kwa muktadha huu Waziri wa mambo ya Nje wa Congo-Brazzaville anatarajia leo Ijumaa kufanya ziara mjini Harare, mji mkuu wa Zimbabwe.

Siku ya Jumatano, alikuwa jijini Lusaka, nchini Zambia ambapo alikutana na rais wa nchi hiyo, Edgar Lungu.

Hata hivyo inasemekana kwamba rais Lungu hatapinga mchakato wa rais Sassou-Nguesso.

Tangu katikati mwa mwezi Machi, matukio mashambulizi yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara kwenye mpaka kati ya DRC na Zambia. Kinshasa inatuhumu jirani yake kwa kutumia ardhi yake na kwa kufanya mara mashambulizi katika nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.