Pata taarifa kuu
DRC-ZAMBIA-USALAMA

DRC yaishtumu Zambia kutaka kudhibiti eneo lake la ardhi

Wiki iliyopita, serikali ya DRC iliishutumu Zambia kwa kutaka kushikilia sehemu yake ya ardhi upande wa majimbo ya Moba na Pweto. Kutokana na hali hiyo serikali ya DRC imeamua kuimarisha uwepo wa jeshi lake kwenye mpaka na Zambia katika maeneo hayo mawili.

Wanajeshi wa Zambia, Agosti 2007 huko Lusaka.
Wanajeshi wa Zambia, Agosti 2007 huko Lusaka. ALEXANDER JOE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mkoa wa Haut-Katanga au ule wa Tanganyika, baadhi ya wabune wameshtumu uwepo wa askari wa Zambia katika ardhi ya DRC.

Katika eneo la Moba, hasa katika vijiji vya Kalubamba na sehemu ya Muliro, ni maeneo yanayokaliwa na askari wa Zambia kwa karibu miezi miwili, kwa mujibu wa vyanzo kutoka serikalini.

"Ninathibitisha kwamba wanajeshi wa Zambia wanashikilia eneo la Kalubamba. Helikopta zinapaa katika anga letu mara mbili hadi tatu kwa siku. Tayari wamechukua kilomita 15 kwenye ardhi ya DRC, " amesema Mwila Lambert, mkuu wa kijadi wa eneo la Moliro.

Huko Pweto, jeshi la Zambia bado halijavuka mpaka wa DRC, vyanzo vya eno hilo vimesema. Lakini zaidi ya wiki moja iliyopita, Zambia ilipeleka vikosi na magari ya kivita kando ya mpaka wake. Hali inayozua hofu upande wa DRC, amesema mjumbe wa shirika moja la kiraia huko Pweto: "Wanajeshi wa Zambia wamepga kambi katika kijiji cha Lupia, mji ulio karibu na mpaka wa DRC. Katika kijiji hicho kuna magari kadhaa ya kivita. Sasa huko, Pweto iko katika hali ya sintofahamu."

Wakati huo huo mamlaka nchini Zambia imefutilia mbali madai hayo ya DRC. "Sio kweli, wana habari ambayo sio ya kweli. Vikosi vya Zambia havijavuka mpaka, viko ndani ya nchi yetu. Vikosi vilivyowekwa kwenye mpaka viko pale kwa kupiga doria wakati kuna tatizo la kusalama; hivyo ndivyo wanafanya hivi sasa, kando na mpaka, wakiwa ndani ya nchi ya Zambia. Miezi miwili iliyopita, askari wa DRC waliingia katika ardhi ya Zambia, walishambulia vijiji na kupora chakula. Hatujui kama walikuwa askari wa DRC au waasi. Sasa ni kwa viongozi wa DRC kuchunguza kwamba walikuwa askari wao au waasi, "Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Joseph Malanji amesema.

"Zambia ina majirani wanane ambao huchangia mipaka. Na haina tatizo lolote na majirani zake saba. Hatuna nia ya kuongeza ukumbwa wa Zambia mbali na mipaka yetu, sisi sio nchi ya aina hiyo, " ameongeza Bw. Malanji .

Mnamo mwaka wa 2011, mzozo mwingine karibu na kijiji cha Moliro huko Moba ulizihusisha nchi hizo mbili. Wakati huo wanajeshi wa Zambia waliwatimua maafisa wa polisi wa DRC na maafisa wa uhamiaji na kupandisha bendera yao, amesema mshauri wa zamani wa wizara ya mambo ya ndani katika mkoa wa zamani wa Katanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.