Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

Kesi inayomkabili Kamerhe kuanza kusikilizwa katika mahakama ya Gombe

Kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Vital Kamerhe inaanza kusikilizwa leo jiini Kinshasa, huku chama cake cha UNC, katika mkoa wa Kivu Kusini kikitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kusususia shughuli za serikali.

Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi.
Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Mshirika huyo wa karibu wa rais Felix Tshisekedi ambaye anazuiwa jela, ameakanusha tuhma dhidi za kufuja Dola Milioni 57 kwa mujibu wa kiongozi wa mashtaka.

Bw. Kamerhe anashtumiwa kupitisha mlango wa nyuma asilimia kumi ya Dola milioni 500 zilizotengwa kwa mpango huo wa siku mia moja wa rais Felix Tshesekedi.

Kesi hii itawashirikisha washtakiwa wengine wawili, Samih Jammal, msimamizi mkuu wa kampuni Samibo Congo Sarl na Husmal Sarl, kampuni ya mafundi wa ujenzi kutoka Uturuki Karmod inayojihusisha na ujenzi wa makazi.

Hata hivyo Mawakili wake Kamerhe wameendelea kukanusha tuhuma dhidi ya mteja wao.

Kulingana na madai ya mwendesha mashtaka, Vital Kamerhe na mfanyabiashara kutoka Lebanon Samih Jammal, kati ya mwezi Machi 2019 na mwezi Januari 2020, walipitisha mlango wanyuma karibu Dola milioni 49. Wawili wanakabiliwa na kifungo hadi miaka ishirini.

Felix Tshisekedi (kulia), kiongozi wa chama cha UDPS na Vital Kamerhe (kushoto), kiongozi wa chama cha UNC, jijini Nairobi (Kenya) Novemba 23 ambapo walifikiana kuunda muungano ... kwa miaka kumi.
Felix Tshisekedi (kulia), kiongozi wa chama cha UDPS na Vital Kamerhe (kushoto), kiongozi wa chama cha UNC, jijini Nairobi (Kenya) Novemba 23 ambapo walifikiana kuunda muungano ... kwa miaka kumi. REUTERS/Baz Ratner
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.