Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

'Mpango wa siku 100 DRC': Kesi ya Vital Kamerhe yaahirishwa hadi Mei 25

Nchini DRC, kesi ya mkurugenzi kwenye Ofisi ya rais nchini DRC Vital Kamerhe imefunguliwa kwa muda ufupi Jumatatu hii, Mei 11, 2020 kabla ya kusitishwa.

Vital Kamerhe, picha ya Novemba 11, 2018 huko Geneva
Vital Kamerhe, picha ya Novemba 11, 2018 huko Geneva Fabrice COFFRINI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerhe anatuhumiwa kupitisha mlango wa nyuma zaidi ya dola milioni 50 kwa jumla ya dola Milioni 500 zilizotengwa kwa mpango wa rais wa "siku 100" .

Baada ya saa moja kesi hiyo ilisitishwa na kutangazwa kwamba imeahirishwa hadi Mei 25 kwa uchunguzi zaidi. Ombi la kutaka kesi hiyo iahirishwe lilitolewa na wanasheria washtakiwa. wamebaini kwamba hawakuweza kupata faili ya wateja wao. Lakini kwa upande wa mashtaka, faili zilikuepo kwenye ofisi ya mahakama.

Alipopewa nafasi ya kujitetea, Vital Kamerhe ameitangaza kwamba aliingilia katika mpango huo kama mkurugenzi wa Ofisi ya rais wa Jamhuri, huku akibaini kwamba walikuwa wasimamizi tisa wa mpango huo wa siku 100, mbali na mratibu wa mpango huu dharura. Vital Kamerhe amesema akisisitiza kwamba kulikuepo na mtego kwenye maswali alioulizwa baada ya kuulizwa aeleze nafasi yake jukumu alilokuwa nalo katika mpango huo.

"Walichagua kile ambacho kitaleta mkanganyiko, hakuna anayeongelea juu ya elimu ya bure katika shule za msingi, kwa mfano," amesema.

Alipoulizwa kuhusu wafungwa wenzake wawili, Vital Kamerhe amekiri kuwa anamtambua mfanyabiashara Samih Jammal kama anavyowatambuwa watu wengi aliokutana nao katika maisha yake, huku akibaini kwamba anamjua Jeannot Muhima kwa jina tu, "na leo ni mara ya kwanza tunakutana naye, " amesema.

Mamia ya watu waliokuwa wamekwenda kusikiliza kesi hiyo katika jela ya Gombe wametawanywa na polisi baada ya saa nne wakisubiri kesi hiyo kuanza, huku waandishi wa habari wakikataliwa kuhudhuria kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.