Pata taarifa kuu
DRC-UN-HAKI-MAUAJI-USALAMA

DRC: Trésor Mputu Kankonde, mmoja wa viongozi wa kundi la Kamuina Nsapu akamatwa

Kesi kuhusu ukweli juu ya mauaji ya wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa mwezi Machi 2017 inaweza kuharakishwa, baada ya mtuhumiwa mkuu katika mauaji hayo Trésor Mputu Kankonde kukamatwa.

Zaida Catalan na Michael Sharp, wataalam wa Umoja wa Mataifa waliouawa nchini DRC.
Zaida Catalan na Michael Sharp, wataalam wa Umoja wa Mataifa waliouawa nchini DRC. RFI
Matangazo ya kibiashara

Trésor Mputu Kankonde, mmoja wa viongozi wa kundi la wanamgambo la Kamuina Nsapu ambaye alikuwa mafichoni kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kusakwa na viombo vya dola nchini DRC, alikamatwa hivi karibuni huko Kananga.

Kukamatwa kwake ni muhimu kwa kuendeleza kesi ya mauaji dhidi ya wataalam hao wa Umoja wa Mataifa, ambayo ilikuwa ikijikokota kwa mwendo wa kinyonga kwa kukosekana wahusika wa mauaji hayo, amesema Gavana wa Mkoa wa Kasaï ya Kati, Martin Kabuya Mulamba.

Trésor Mputu Kankonde alikamatwa usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi nje kidogo ya mji wa Kananga. Vyanzo vya jeshi vinabaini kwamba alianguka katika mtego wa idara ya ujasusi ya jeshi baada ya kusakwa kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwa mujibu wa mwanasheria Trésor Kabangu kutoka Kananga, mashuhuda wengi wanamuona kama sehemu muhimu katika kutafuta ukweli juu ya kuuawa kwa wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa, Zaïdan Catalan na Michael Sharp mwezi Machi 2017.

Jean-Bosco Mukanda, shahidi mtuhumiwa ambaye anazuiliwa akihusishwa katika kesi hiyo in ayoendelea huko Kananga, awali alitangaza mbele ya majaji kuwa Mputu Kankonde ndiye ambaye alichukuwa nywele za Zaïdan Catalan.

Lakini njama kati ya kiongozi huyu wa wanamgambo wa kundi la Kamuina Nsapu na maafisa wengine wa idara ya ujasusi ilisababisha kiongozi huyo kuchelewa kukamatwa, vimebaini vyanzo rasmi.

Chanzo cha usalama pia kinadai kwamba wakati wa kukamatwa kwake, Trésor Mputu Kankonde alikuwa akijaribu kupanga tena wanamgambo wa kundi la Kamuina Nsapu kwa lengo la kushambulia mji wa Kananga kutoka mji wa Kasuyi.

Kulingana na mkuu wa mahakama ya kijeshi Jean-Blaise Bwamulundu, Trésor Mputu Kankonde atafikishwa mahakamani hivi karibuni. Washtakiwa ishirini na nne bado wako wanazuiliwa jela, watatu wamefariki dunia na wawili wamatoroka katika mazingira tatanishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.