Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

DRC: Vital Kamerhe asalia kororokoni

Mkurugenzi katika ofisi ya rais Felix Tshisekedi, Vital kamerhe ataendelea kusalia jela kulingana na uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kinshasa Jumatano jioni wiki hii.

Vital Kamerhe, mkuu wa serikali na mshirika mkuu wa kisiasa wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi, aliwekwa kwa muda kizuizini katika gereza kuu la Kinshasa wakati wa uchunguzi wa kazi ya siku 100.
Vital Kamerhe, mkuu wa serikali na mshirika mkuu wa kisiasa wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi, aliwekwa kwa muda kizuizini katika gereza kuu la Kinshasa wakati wa uchunguzi wa kazi ya siku 100. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerhe, mshirika wa karibu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alikamatwa hivi karibuni, kwa madai ya ufisadi, baada ya mahakama kukataa kuachiliwa kwake licha ya shinikizo kutoka kwa chama chake cha UNC.

Baadhi ya mashirika kama vile ODEP au AMKA yanashuku kuwa pesa nyingi zilipitishwa mlango wa nyuma. Ikiwa Vital Kamerhe anakabikliwa na mashitaka hayo, ni kwa sababu yeye sio tu "afisa anayesimamia masuala ya gharama katika opfisi ya rais, lakini pia, kwa sababu hadi Septemba 2019, alikuwa anasimamia kwa mkono wa chuma fedha za mpango huo ”, vyanzo kutoka ofisi ya mashtaka, na vile kutoka kambi ya mshirika wake, Félix Tshisekedi vimebaini.

Watu kadhaa walikamatwa mwezi Machi mwaka jana kufuatia madai hayo, huku viongozi wa makampuni ya kibinafsi na yale ya umma wakiwekwa korokoroni kabla ya kuachiliwa huru.

Kukamatwa kwa Vital Kamerhe nchini DRC kumesababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama chake cha UNC.

Vital Kamerhe (alizaliwa 4 Machi 1959) ni mwanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kiongozi wa chama cha UNC.

Alikuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwaka 2006 hadi 2009. Kabla ya hapo alikuwa Waziri wa Habari.

Baada ya kujiuzulu kama spika wa Bunge, alikuwa mpinzani na kuanzisha chama cha UNC. Alikuwa mgombea katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2011.

Tarehe 8 Aprili 2020, Vital Kamerhe, mkuu wa serikali na mshirika mkuu wa kisiasa wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi, aliwekwa kwa muda kizuizini katika gereza kuu la Kinshasa wakati wa uchunguzi wa kazi ya siku 100 baada ya rais Tshisekedi kuchukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.