Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-SIASA

Kukamatwa kwa Vital Kamerhe DRC kwasababisha mgawanyiko ndani ya chama cha UNC

Mahakama ya Kinshasa inatarajia kutoa uamuzi wake Jumatano, Aprili 15, kuhusu ombi la Vital Kamerhe la kuachiliwa kwa dhamana. Mkurugenzi kwenye ofisi ya rais wa DRC anakabiliwa na madai ya ufisadi.

Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi.
Vital Kamerhe alisimamia mpango wa dharura kwa siku 100 za kwanza katika serikali ya rais Tshisekedi. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii imezua sintofahamu ndani ya chama chake cha UNC mpaka kufikia Vital Kamerhe kuwataka wafuasi wake na viongozi wengine wa chama wasizungumze bila idhini yake.

Kwa upande wa baadhi ya makada wa chama cha UNC, kesi hii inakusudia kumuondoa Vital Kamerhe katika kinyang'anyiro cha urais cha mwaka 2023. Uchaguzi ambao Félix Tshisekedi atamuunga mkono Vital Kamerhe kuwania kulingana na makubaliano, yaliyotiliwa saini jijini Nairobi, nchini Kenya, kati ya vyama vya UNC na UDPS.

Wengine wanasema, "rais wa sasa ametoa kafara mshirika ambaye wanaamini anashikilia siri za madaraka yake."

Washirika wa karibu wa Félix Tshisekedi wameumizwa sana na kauli hizi tofauti, hasa kwani baadhi ya kauli zilitolewa na watu ambao bado wanafanya kazi katika ofisi ya rais wa sasa.

Pia Vital Kamerhe mwenyewe hakufurahishwa na kauli hizo, ambaye kwa mujibu wa washirika wake, anaendelea kuamini kwamba suluhisho la kisiasa linaweza kupatikana bila kuingia katika malumbano na chama cha UDPS. Chama cha UNC bado hakifikirii kuvunja muungano na chama cha rais, wamesema.

Kufikia sasa, hakuna kada wa chama hata mmoja aliyemtupilia Vital Kamerhe, chanzo kingine cha chama cha UNC kimebaini. Wengine wanasubiri matokeo ya kesi. Wengine hujipa muda kabla ya kuchukua uamuzi wa mwisho, ameongeza afisa mmoja wa serikali, mfuasi wa chama cha UNC. Kwa sasa, Vital Kamerhe anaongoza chama chake akiwa kizuizini, huku akipokea ujumbe kutoka kwa wafuasi wake na kuzungumza na washirika wake kila siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.