Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

DRC: Vital Kamerhe awekwa kizuizini baada ya kusikilizwa kwa masaa 6

Mkurugenzi kwenye ofisi ya rais Félix Tshisekedi, Vital Kamerhe, yuko kizuizini baada ya kutolewa waranti wa kukamatwa Jumatano hii jioni Aprili 8, na kuhamishiwa katika gereza la Makala.

Vital Kamerhe (hapa ilikuwa Novemba 11, 2018 huko Geneva) anazuiliwa katika gereza la Makala.
Vital Kamerhe (hapa ilikuwa Novemba 11, 2018 huko Geneva) anazuiliwa katika gereza la Makala. Fabrice COFFRINI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Alisikikizwa kwa madai ya ya kupotea kwa pesa zilizotengwa kwa mpango wa dharura wa rais wa DRC.

Vital Kamerhe aliambatana na wanasheria wake wawili katika ofisi ya mashitaka saa saba mchana baada ya kukutana na umati mkubwa wa wafuasi wake waliokuwa wamekwenda kumuunga mkono kiongozi wao. Bw Kamerhe alisikilizwa kwa muda wa masaa sita kuhusu jukumu lake katika usimamizi na utekelezaji wa fedha zilizotengwa kwa mpango wa dharura wa rais unaitwa "siku 100" uliozinduliwa na Rais Félix Tshisekedi mwezi Machi 2019, miezi miwili baada ya kuapishwa kwake kama rais wa DRC.

Mashirika yasiyo ya kiserikali, lakini pia mashirika ya kiraia wanashutumu ofisi ya rais kutoa zabuni kwa upendeleo bila kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Baadhi ya mashirika kama vile ODEP au AMKA yanashuku kuwa pesa nyingi zilipitishwa mlango wa nyuma. Ikiwa Vital Kamerhe anakabikliwa na mashitaka hayo, ni kwa sababu yeye sio tu "afisa anayesimamia masuala ya gharama katika opfisi ya rais, lakini pia, kwa sababu hadi Septemba 2019, alikuwa anasimamia kwa mkono wa chuma fedha za mpango huo ”, vyanzo kutoka ofisi ya mashtaka, na vile kutoka kambi ya mshirika wake, Félix Tshisekedi vimebaini.

"Katika kipindi chote alipokuwa akisikilizwa, hakutoa ushahidi wa kutosha na hakuwashawishi waendesha mashitaka," chanzo cha mahakama kimeiambia RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.