Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI-UFISADI-SIASA

Kesi ya kupotea kwa dola Milioni 15 DRC: Ofisi ya rais yanyooshewa kidole

Kesi hii ya kupotea kwa Dola Milioni 15 imezua hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku mashirika ya kiraia yakiomba uchunguzi wa kina ufanyike ili kupata ukweli wa mambo.

Vital Kamerhe (kushoto) na Rais Felix Tshisekedi katika hafla ya kutangazwa kwa muungano wao jijini Nairobi Novemba 23, 2018.
Vital Kamerhe (kushoto) na Rais Felix Tshisekedi katika hafla ya kutangazwa kwa muungano wao jijini Nairobi Novemba 23, 2018. © AFP/Yasuyoshi Chiba
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo wakosoaji wa Mkurugenzi wa ofisi ya rais, Vital Kamerhe, wanamuhusisha kiongozi huyo kwa kesi hiyo, licha ya yeye kufutilia mbali tuhuma hizo.

Kupotea kwa fedha hizo kumeibua maswali mengi kati ya mashirika mbalimbali na wakosoaji wa serikali ya DRC.

Vital Kamerhe ambaye wakosoaji wake wanamwita "rais wa pili" amepuuzia mbali madai hayo akisema kuwa lengo la wapinzani wake ni kumchafua tu.

Vital Kamerhe ni miongoni mwa viongozi wanne ambao Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali unawahusisha katika kesi hiyo ya kupotea kwa dola Milioni 15.

Mwezi mmoja na nusu baada ya kesi hii kuanza, Rais Felix Tshisekedi, hajatoa tamko lolote kuhusu suala hilo. Ukimya ambao wanaharakati wa mashirika ya kiraia wanalaani.

Wanaharakati hao wanamkubusha Rais Tshisekedi kuhusu ahadi yake ya kupambana dhidi ya ufisadi kuwa ni moja wapo ya vita kwa muhula wake.

RFI imepata uthibitisho kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka kwenye Mahakama ya Juu, iliyokabidhiwa kesi hiyo Julai 31 na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali, tayari imefungua uchunguzi wa awali. Katika mahojiano na Gazeti la Jeune Afrique, Vital Kamerhe, Mkurugenzi wa ofisi ya Rais Félix Tshisekedi, amefutilia mbali kuhusika kwake katika kesi hiyo na amekanusha suala la "kupotea kwa fedha hizo", na kusema kuwa kesi hiyo "imesitishwa" na Mkaguzi Mkuu wa kitengo cha Uhalifu wa Uchumi.

Vital Kamerhe pia alisitisha uchunguzi mwingine uliozinduliwa na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (IGF), ikiwa ni pamoja na uchunguzi kuhusu matumizi yote kwenye wizara mbalimbali tangu Felix Tshisekedi kuchukuwa madaraka, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka serikalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.