Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA-HAKI

DRC: Vital Kamerhe aitishwa na ofisi kuu ya mashtaka, chama chake chalaani

Mkurugenzi mkuu kwenye ya ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vital Kamerhe ameitishwa na ofisi kuu ya mashtaka jijini Kinshasa, ambayo inachunguza madai ya ufisadi wa fedha zilizotengwa kwa mpango wa dharura wa rais wa DRC.

Vital Kamerhe, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi.
Vital Kamerhe, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerhe ambaye anasimamia utekelezaji wa shughuli hiyo anakabiliwa na mashitaka makubwa ambayo wengi wanaona kuwa yanaweza kumkosanisha na rais Félix Tshisekedi.

Watu kadhaa walikamatwa mwezi Machi mwaka jana kufuatia madai hayo, huku viongozi wa makampuni ya kibinafsi na yale ya umma wakiwekwa korokoroni kabla ya kuachiliwa huru.

Kuitishwa kwa Vital Kamerhe kuripoti mbele ya ofisi kuu ya mashitaka kunawatia wasiwasi wafuasi wake pamoja na washirika wake wa karibu. Mawaziri, washauri wa rais na wajumbe wengine wa baraza la mawaziri walikusanyika Jumapili kulaani kile walichokiita "vurugu" na "kampeni ya mbaya dhidi ya kiongozi wao inayolenga kuharibu muungano wa vyama vinavyo muunga mkono rais Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.